@chrisnewstv: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amempongeza Jacki Mngoni kwa kupaza sauti kuhusu video ya faragha ya mtoto inayosambaa mitandaoni, huku akiwataka watu kuacha kuisambaza na badala yake kuiwasilisha kwa Dawati la Jinsia la Polisi. Kupitia ujumbe wake, Gwajima amesema hajaitazama video hiyo na hana nia ya kuiona, akisisitiza kuwa anayemiliki video hiyo anapaswa kuikabidhi Polisi kupitia namba 0699 913 200. Aidha, amemtaka binti anayehusika kuripoti tukio hilo Polisi au Ustawi wa Jamii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mtu anayehusika na ukatili huo. Waziri huyo ameeleza kuwa mhusika (mwanaume) anaweza kukabiliwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka 10 na faini ya hadi Sh milioni 20, au adhabu zote mbili kwa pamoja, kwa mujibu wa sheria. Pia ameomba apewe taarifa za shule anayosomea binti huyo ili wizara iweze kushirikiana na walimu katika kufuatilia suala hilo na kusaidia kumpata mtuhumiwa. Dkt. Gwajima amesisitiza ujumbe mmoja: TUACHE KUSAMBAZA VIDEO HIYO, TUWALINDE WATOTO NA TUACHE SHERIA IFANYE KAZI#chrisnewstv #1millionviews

CHRIS NEWS TV
CHRIS NEWS TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 10 November 2026 15:31:52 GMT
3108
28
0
3

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @chrisnewstv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About