@almecky_tz: Tanzania na Oman zimeweka lengo la kuongeza thamani ya biashara kati ya nchi hizo kutoka Dola za Marekani milioni 389 za sasa hadi Dola bilioni moja ifikapo mwaka 2030. Lengo hilo limetangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, baada ya nchi hizo kusaini mikataba 14 ya ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo. Kombo amesema mikataba hiyo inalenga kuongeza fursa za biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Oman. Aidha, amesema Oman imetoa ufadhili wa masomo 160 kwa Watanzania katika nyanja mbalimbali za elimu ili kuongeza fursa za kielimu na ujuzi wa wataalamu nchini. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Joseph John Kilangi, amesema ushirikiano huo unatarajiwa kuinufaisha Zanzibar katika sekta ya nishati kupitia utaalamu na uzoefu wa Oman. Mikataba hiyo imesainiwa katika Mkutano wa Tatu wa Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman uliofanyika Zanzibar. #Zanzibar #Tanzania #Habari #Football #Trending

almecky_tz
almecky_tz
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 10 November 2026 16:18:54 GMT
6445
242
10
47

Music

Download

Comments

zinjibar.44440
zanzibar ❤️zaman :
zinjibar ♥️Oman
2026-11-10 23:49:20
1
grizzy_dark
grizzy dark :
mbona sis hatujui
2026-11-10 21:32:07
0
lamu3770
Lamu :
Tunarudi nyumbani
2026-11-10 22:43:01
0
bazaar997
BAZAAR :
Jamani gesi ipo Ardhini si mchimbe mzalishe umeme😅
2026-11-11 03:42:29
0
afsheenrahim297
afsheenrahim297 :
huyu MH. ninawasiwasi na maelezo yke anajaribu kuficha UKWELI
2026-11-10 18:59:05
0
amouralhanjary
user650854274132 :
hongera mheshimiwa kwa jitihada zako za kuwaunganisha waoman na watanzania sisi tunaudugu wa damu
2026-11-10 18:28:31
0
grizzy_dark
grizzy dark :
ila cc tz c broila
2026-11-10 21:29:03
0
afsheenrahim297
afsheenrahim297 :
kuweni makini na waomani kwao maisha magumu wasije kupora ardhi yetu
2026-11-10 18:56:30
0
user325312761736
اليعربي :
Munazidi kututawala tu Wabara
2026-11-10 18:49:34
0
aziza.aziza3640
❤❤my baby❤ :
🥰🥰🥰
2026-11-10 17:57:51
0
To see more videos from user @almecky_tz, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About