@nmmediatv: Tukio lisilo la kawaida limeripotiwa kutokea baada ya Mtanzania aliyekuwa akifanya kazi ya kuendesha mashine katika kampuni inayomilikiwa na raia wa China kudaiwa kuharibu mali za mwajiri wake kufuatia kutolipwa mshahara wake kwa kipindi cha miezi mitatu. Kwa mujibu wa taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mfanyakazi huyo alikuwa akidai malipo ya kazi aliyokuwa akiifanya, lakini kila alipomuuliza mwajiri wake kuhusu mshahara, alielezwa kuwa atalipwa atakapojidhihirisha na kuthibitisha uwezo wake wa kufanya kazi. Inadaiwa kuwa baada ya kukosa uvumilivu, mfanyakazi huyo aliamua kuchukua hatua hiyo ya kuharibu mali za kampuni, huku video ikimuonesha akiwa na mashine ya kuchimbia akiharibu gari lililokuwa eneo la tukio. Hata hivyo, chanzo halisi cha tukio hilo na hatua zilizochukuliwa na mamlaka bado hazijafahamika.