@jambotv_: VIDEO: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Clement Sangu, amesema Serikali imebaini utekelezaji wa agizo la kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi kufikia takribani asilimia 90. Hata hivyo, amesema baadhi ya waajiri bado hawajatekeleza kikamilifu agizo hilo, hivyo Serikali inatarajia kuwaita waajiri wa sekta husika mwanzoni mwa mwezi Desemba ili kuhakikisha wanazingatia matakwa ya sheria. Sangu ameyasema hayo leo Novemba 11, 2026, jijini Arusha, wakati akifungua semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), akisisitiza kuwa waajiri watakaobainika kukiuka sheria watachukuliwa hatua stahiki. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Rugemalila Rutatina, amesema miongoni mwa changamoto zinazotukabili vyama vya wafanyakazi ni kuanzishwa kwa vyama vidogo vinavyotokana na migogoro ya uongozi ndani ya vyama vikubwa, hali inayochangia migogoro na kudhoofisha utendaji wa taasisi. Aidha, Rutatina ameitaka Serikali kutoa mwongozo kuhusu changamoto hizo, huku akibainisha kuwa baadhi ya taasisi hazitekelezi ipasavyo matakwa ya kisheria ya kuunda na kuendesha mabaraza ya afya na usalama kazini, jambo linalohitaji kupewa kipaumbele ili kulinda ustawi wa wafanyakazi. Ikumbukwe kuwa Serikali ilitoa Amri ya Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi ya mwaka 2025, iliyopandisha wastani wa kima hicho kwa asilimia 33.4 kutoka Shilingi 275,060 hadi Shilingi 358,322 kwa mwezi, huku viwango vikitegemea sekta husika

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 11 November 2026 17:49:48 GMT
40249
883
73
87

Music

Download

Comments

sulley1462
sulley :
aweke no yake tumweleze wenyew shida tunazopitia
2026-11-12 11:23:29
7
pikrean.www
PRIEST FESTO SILLA :
kampuni za ulinzi na za usafi...bado sana hawajaongezewa mshahara
2026-11-12 03:36:18
10
user9012792526128
Saidi J Nkrumah :
ni kweli mh anza na kampun za ulinz asa suma na makampun mengine
2026-11-11 18:01:31
8
vivianelivis
vivianelivis :
mungu nakuomba na hii kampuni yangu ipitiwe watakapo Anza huo uchunguzi maan Kuna muda nakosa hadi nauli ya kwenda kazini baba wa binguni tutete sisi wote tunaofanya kazi kwenye makampuni 🙇🙇🙏🙏
2026-11-12 09:18:00
4
user6218361240685
motisha :
weweeeeee mambo yanakaribia kuwa byeeeeeeeeeee
2026-11-12 07:31:19
0
john.kimatari
nunda🤫🤫💯 :
Na omba tamko hili lije moshi
2026-11-12 07:50:20
1
user62610630081381
BILLY ⚓ :
badala ya kufika kwenye miradi na makapuni muhoji wafanya kazi na wajiri muachukulue hatua kwenye maeneo Yao mnataka kuita kikao nao ili mpate bajeti tokeni muende kwenye maeneo Yao mukajione tasisi za kazi nchini wajui jukumu Lao wanakaa Tu officen ukipeleka lalamiko lako kuhusu masilai yako ukirudi kazini huna kazi rushwa Tu imetawala
2026-11-12 17:54:28
1
user2566285472450
user2566285472450 :
shida ya hii serikali sio wafuatiliji kabisa ndiyo maana wanafanya wanavyotaka
2026-11-12 16:46:06
1
.rose50691
@🌹 :
USISAHAU HIZI INTERNATIONAL COMPANY (PRIVATE MUNGU ANAWAONA)
2026-11-12 13:57:09
0
gpetrouswege1995
g@petrouswege1995 :
mbona kwenye makampuni ya ulinzi wanalipa 130000 kwa mwezi??????
2026-11-12 13:59:16
0
peter.severini
peter severini :
Hakika makampuni za ulinzi ni shidaaa sana hasa ws insight security
2026-11-12 04:11:21
3
badobuku23
MTPD 🇹🇿 :
Sio sekta binafsi peke yao hadi Halimashauri kima chamshahara kipo chini sana hakuna posho mishahara midogo pitieni tena hayo marizio haswa vituo vya afya haswa walizi wanapitia halingumu sana wana madeni kila kona agizo halifanyiwi kazi katika sekta na taasisi za uma
2026-11-12 14:40:23
1
shaffy.mabuyu
Shaffy Mabuyu :
kwani ndomnaanza kujumbusha baada tukio au kablatukio mm sijaelewa
2026-11-12 12:40:58
1
user8282168432069
deogratus mlai :
viwanda vyote wanalipa sh Elfu 7 kwakutwa
2026-11-12 11:51:47
1
user803709394325
paul patrick masanja :
hakuna jipya kweny hili mana wajli mnawaogpa hamna anaye fatilia
2026-11-12 10:40:48
1
priscamnzava537
Prisca Mnzava :
amkuu anza na suma jkt gurd na makampuni mengine
2026-11-12 11:00:01
1
thomasmalaki
thomasmalaki :
mkuu, fuatilia ajira za track drivers . huko ndio changamoto zaidi.
2026-11-12 06:08:12
1
user6908354573111
nakanganigwe :
kuna tass zingine amuziwezi kuziwajibisha
2026-11-12 06:27:46
0
annastazia.annast49
AN :
naomba kujua kima cha chin
2026-11-12 17:47:17
0
user2566285472450
user2566285472450 :
waiteni mpaka makampuni ya utalii Kuna shida kubwa huku
2026-11-12 16:44:18
0
user33687418330
user33687418330 :
inshaallah mungu tufanyie wepesi kwa ilo
2026-11-12 20:05:33
0
matibaa
MR TIMOTHY :
Mimi nitangulieee mba mama samiaa azingatiee hayaa tunateseka sana
2026-11-12 17:00:11
0
user2471691880299
user2471691880299 :
Mlosema shilingi ngapi vile???
2026-11-12 17:22:16
0
piusmuhanuzi
CHEUPE TRADERS :
Shida nani anafuatiria kuhakiki utekelezaji!?
2026-11-12 17:02:59
0
sherrymsomali819
Sherry msomali :
mahoteli mheshimiwa humo ndio mwakuwanza
2026-11-12 16:47:22
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About