@tangavision1: TANGA: BEI YA MAJI YAONGEZEKA, TANGAUWASA YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHIWA MAJI Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA) imetangaza ongezeko la bei ya maji kwa wateja wake kutoka Shilingi 1,931 hadi Shilingi 2,625 kwa kila mita ya ujazo. Ongezeko hilo limeidhinishwa na EWURA, huku likiwa chini ya kiwango cha Shilingi 3,000 kilichoombwa na TangaUWASA. Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Tanga, Meya wa Jiji, Mhe. Seleboss Mustafa, ameeleza kuwa pamoja na mabadiliko hayo, TangaUWASA imepunguza gharama za kuunganishiwa maji kutoka bomba kuu hadi kwa mteja. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, gharama ya kuunganishiwa maji sasa ni Shilingi 26,000, huku mteja akitakiwa kununua vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya ufungaji. Hatua hiyo inalenga kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi, taasisi za Serikali na taasisi za dini, pamoja na kuiwezesha TangaUWASA kuimarisha huduma zake. SWALI KWA WANANCHI WA TANGA: Una maoni gani kuhusu ongezeko la bei ya maji kutoka Sh 1,931 hadi Sh 2,625 kwa mita ya ujazo, huku gharama ya kuunganishiwa maji ikipunguzwa? Je, hatua hii italeta nafuu kwa wananchi? 📍 TANGA YETU, MAENDELEO YETU. #TangaVision #Tanga #TangaUWASA #MaendeleoYaTanga #Maji
Tanga Vision
Region: TZ
Thursday 12 November 2026 16:52:48 GMT
Music
Download
Comments
muodally :
ccm nayo inasemaje
2026-11-13 07:31:21
0
mudrck :
nchi ngumu sana uku twaambiwa cement yashuka uku maji yapanda uku watu waambiwa walinde migongo duh
2026-11-12 18:09:48
2
Mabango_3D :
Maji Ni UHAI kwaiyo Mnatupandishia Gharama ya Uhai wetu au Sio.... Sawa bana ila Hatutakufa Kwa KIU
2026-11-13 07:43:29
0
user4048254971700 :
hapo bei haija panda nimitihani je kweli tutaweza kweli jamani? hyo bei mpya
2026-11-13 06:35:54
0
user2000958476997 :
mupandishe bei maji ni yenu ama ya Allah.
2026-11-13 05:23:43
0
Ally Shael :
serikali zetu za kiafrika ni kukandamiza tu wananchi wallah
2026-11-13 05:33:03
0
💜 :
punguzeni hali sizo jua kali sana
2026-11-12 20:15:54
0
The_Meeck :
Wangese
2026-11-12 20:48:42
0
Thomas Mathew :
twaafa
2026-11-12 18:51:23
0
D~Momo Officially🤱💞 :
babu
2026-11-12 18:49:18
0
Ek mom93 :
mh
2026-11-12 19:15:28
0
To see more videos from user @tangavision1, please go to the Tikwm
homepage.