@wizarayamifugonau: *DKT. BASHIRU : TUNATAKA KUKOMESHA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI* Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema serikali haitamvumilia mtu yeyote atakaye kwamisha malengo ya uzalishaji wa chakula na kwamba suala migogoro ya wakulima na wafugaji linapaswa kuratibiwa Kitaifa ii kukomesha tatizo hilo. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Amesema baada ya tatizo hilo kuenea na kuanza kutishia amani na usalama katika sekta za kilimo na mifugo, Waziri Mkuu ameunda timu ya Wizara Nane, ambapo ya wataalam imeanza kufanya uchambuzi wa kiini chake ili kuisaidia serikali katika kulikomesha suala hilo. Aidha, amesema mtu yeyote atakayefanya kosa haijalishi nafasi, kazi na nyadhifa yake achukuliwe hatua kali za kisheria kama mhalifu mwingine na kwamba kosa mtu mmoja awe mfugaji, mkulima au kiongozi huku akisisitiza kuwa serikali haitakubali kuendelea kuona migogoro hiyo. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ametoa Kauli hiyo leo Tarehe 12 Novemba 2026 katika eneo la Mangaka Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wakati wa Ziara ya Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Mtwara, ziara inayolenga kukagua ukaguzi wa Miradi ya serikali. Hata hivyo serikali imeendelea kuhimiza uzingatiaji wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inayohumiza kupanga matumizi bora ardhi kwa ajili ya wakulima, wafugaji, uwekezaji hatua itakayosaidia kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Wizarayamifugonauvuvi
Region: TZ
Friday 13 November 2026 03:11:44 GMT
Music
Download
Comments
Masinga Jr :
Wewe ni kiongozi
2026-11-13 04:35:40
0
To see more videos from user @wizarayamifugonau, please go to the Tikwm
homepage.