@pimango_sports_one: Mchezaji Pacome ameanza hatua nyingine muhimu katika safari yake ya kurejea uwanjani baada ya kuonekana akifanya mazoezi maalumu ya kurejesha uwezo wa mwili. Katika hatua hii, Pacome amefanya mazoezi ya kutembea na kukanyaga chini kwa utulivu, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kurejesha uwezo wa mguu kabla ya kuanza hatua inayofuata ya mazoezi ya kukimbia. Hatua hii ni sehemu ya rehabilitation process, inayolenga kumsaidia mchezaji kurejesha uwezo wa kutembea, uimara na utendaji wa mguu hatua kwa hatua, huku akiepuka kuharakisha kurejea kwenye mazoezi mazito. Mashabiki wanaendelea kusubiri kwa hamu maendeleo ya Pacome kuelekea kurejea kwenye ushindani.