@uhuruonline: #HABARI : SALEH Khamis Baseleman, anayefahamika kwa jina la Mbwiga, anayedaiwa kuongoza mtandao wa kimataifa wa biashara, usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya, amekamatwa nchini Kenya. Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumefuatia operesheni maalumu ya kimataifa iliyoratibiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya nchi husika. Operesheni hiyo ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya inayovuka mipaka ya nchi, huku ikilenga kubaini na kuvunja mitandao ya wahalifu wanaojihusisha na shughuli hizo. Ushirikiano huo wa kimataifa unalenga kudhibiti usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na kuimarisha juhudi za kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka ya nchi. #uhuruonline #uhuruupdates

uhuruonlinetz_
uhuruonlinetz_
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 13 November 2026 08:42:10 GMT
11623
257
9
80

Music

Download

Comments

black.british.pyr
Mohamed Nzallah :
haswaa zinapitaje .
2026-11-24 04:33:34
0
smartness_sofa
Smartness_sofa :
kazi nzurii sanaa vizazi vyetu vinaangamia mitaani
2026-11-13 10:37:31
2
bawesaspiritual13
BawesaSpiritual#13 :
kazi nzuri ila utatumbuliwa mzee
2026-11-13 11:47:03
2
weda.ndunda.wdzain
weda ndunda @WDZAINI17 :
kazi nzuri ila hapo kwenye belya panashida panahaja kupaangaria kupaangaria
2026-11-13 14:24:16
0
ramadhanisharifu
Ramadhani Sharifu :
bwiga Gani jamani hiyo wa zanziba
2026-11-13 20:50:05
0
mpemba144
Mpemba1 :
Duuu
2026-11-14 18:47:57
0
le.moment.de.zanzibar
le moment Tours & Expérience :
umeme una zimwaa😂
2026-11-21 19:41:35
0
dangote.tz55
dangote tz :
ajali kazin
2026-11-13 14:13:55
0
dieu.aime.bwenge
Dieu aime bwenge Destin :
😁😁😁
2026-11-14 21:04:19
0
To see more videos from user @uhuruonline, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About