@millardayo_: Huduma mbalimbali za kampuni ya teknolojia ya Microsoft, zikiwemo Outlook, Teams na Copilot, zimeripotiwa kukumbwa na hitilafu kubwa iliyodumu kwa takribani saa 12, na kuathiri maelfu ya watumiaji nchini Marekani pamoja na shughuli za kibiashara katika Nchi za Asia na Pasifiki. Hitilafu hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 13, 2026 imeripotiwa kuathiri Taasisi za Serikali nchini Marekani, Australia na Japan, pamoja na kampuni zinazojihusisha na teknolojia ya akili bandia (AI), zikiwemo OpenAI na Anthropic. Kwa mujibu wa tovuti ya Downdetector inayofuatilia hitilafu za huduma za mtandaoni, zaidi ya taarifa 130,000 za matatizo ya Outlook ziliripotiwa nchini Marekani katika kilele cha hitilafu hiyo siku ya Alhamisi, huku changamoto nyingine zikiripotiwa India, Australia na Japan. Microsoft imesema imefanya marekebisho katika seva zilizoathirika, ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Australia, Tony Burke, amesema Microsoft inaamini hitilafu hiyo huenda ilisababishwa na tatizo katika maboresho ya mfumo, linalofanana na hitilafu iliyohusisha kampuni ya CrowdStrike mwaka 2024. #MillardAyoUPDATES

millardayo
millardayo
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 13 November 2026 11:20:53 GMT
222879
12507
684
304

Music

Download

Comments

__.divah_
Shop with Divah🛍 :
Elon anahusika😂😂😂kasema atainunua kumnyamazisha Billgate🤦‍♀️
2026-11-13 11:56:38
74
ayoubjo2
Job Nestory 🫂🧑‍🤝‍🧑 :
Lakin si Haiusiani na Mambo ya Msosi Ety🤔
2026-11-13 11:34:27
563
nargis8131
hanimay🥰🥰 :
iy Microsoft mm nmesoma ziaribke tuu kwanz ajra zenyew hakuna bwan[Big LOL][Big LOL]
2026-11-14 05:30:56
0
liylagirl
Liyla :
mtu anieleweshe Microsoft ndonini
2026-11-13 11:24:09
243
obbymick
Obby michael :
Microsoft ni kampuni kubwa ya kimataifa ya teknolojia ya habari (Information Technology) iliyoanzishwa mwaka 1975 nchini Marekani na Bill Gates pamoja na Paul Allen. Kampuni hii inajihusisha na kutengeneza, kuendeleza na kusambaza programu za kompyuta, mifumo ya uendeshaji (Operating Systems), huduma za mtandao na teknolojia za kisasa. Microsoft inajulikana zaidi kupitia bidhaa zake kama Microsoft Windows kwa ajili ya kuendesha kompyuta, Microsoft Word kwa kuandika na kuhariri nyaraka, Microsoft Excel kwa kufanya mahesabu na uchambuzi wa taarifa, Microsoft PowerPoint kwa kuandaa mawasilisho ya kitaaluma, pamoja na Microsoft Outlook kwa mawasiliano ya barua pepe. Kwa ujumla, Microsoft ina mchango mkubwa katika kurahisisha shughuli za elimu, biashara, mawasiliano, usimamizi wa taarifa na maendeleo ya teknolojia duniani.
2026-11-13 12:08:25
165
lindas.loyal
Linda's Loyal :
Dear Customer, due to a Microsoft service outage, email and OTP services are temporarily unavailable. We apologise for any inconvenience caused. For more info, call 0800780111. mi nimepata hii kutoka exim bank najiuliza tu kwani kule Paraguay ilikuwaje bank ikazama na pesa zote, 😳 ama ninywe chai kwanza niamke aha nachoka mimi
2026-11-14 08:06:17
0
zane_ch5
🫧Zane🧸 :
vile wenye wanatumia darkweb wanatuona
2026-11-13 11:28:48
39
derickleonard671
Rick champ🥊🥊 :
hacker mafia washasababisha duuuuuuuu
2026-11-14 04:01:52
0
user7209831030299
auntie :
jamani we kaka[Tears of joy][Tears of joy]
2026-11-14 07:57:08
0
its.zuhura.maria
it's zuhura maria🦋 :
Uzuri Elon Musk alimwambia Bill gate atanunua Microsoft ili kumfukuza kazi 😂😂
2026-11-14 03:29:57
8
samwelabdallah732
m'yau :
ndomaan cm yangu ilikuwa inaniletea wanyarugusu😂
2026-11-13 12:06:37
51
kaynashy2
Kaynashy :
nilitak nishangae kwnn yavurugike maisha yng tu[Tears of joy][Tears of joy]
2026-11-13 12:51:09
15
mama.j194
~Dee♥️ :
ndo maan Leo network sielew
2026-11-13 20:32:13
0
s.h.a.m.i.m.a.82
Tanga girl🌸🍁🕊 :
kuna mtu kasema si haihusiani na maswala ya msosi ety
2026-11-13 18:24:45
15
molife41
MO_Life :
nd microphone test au
2026-11-13 11:59:03
0
misskunduchi1
Miss Kunduchi💅 :
uku nachanganywa na maisha yangu na mahusiano yangu nikajua nikija uku nitapumzika ndo mwazindi kunichanganya zaidi😳haya MICRSOFT ndo kitu gani???
2026-11-13 13:20:58
11
isasibisaku
isasi bisaku :
kuna utabiri wa mwisho wa dunia kuwa leo nani anajua hii?
2026-11-13 12:02:33
50
mamujarry
Maryam🦋 :
microsoft word au
2026-11-13 12:22:30
3
mama.triple.stans
Mama triple :
Lakin pesa zetu bank mtatupa tu hata kama microwave zenu hazisomi
2026-11-13 13:12:07
5
a2peace
Dr. vision 🔮 :
Kwaivyo kwanzia leo hakuna kadi za kuchangishana kwenye masherehe sio😂😂😂
2026-11-13 12:16:15
8
azamo_delivery
Azamo_delivery :
Hakikisha lile deni langu lishapotea kwenye database ya boss wangu baada huo mvurugiko😂
2026-11-13 11:54:31
19
moonation1
Mods Dickson☑️ :
ndo maana songesha wameniongezea deni
2026-11-13 12:33:09
7
ruthlinaeliah240
Teejal🩵 :
microsoft ni nn tena 🙄
2026-11-13 11:25:01
5
m3gan681
M3GAN :
watajua wenyew sisi 2na 2mia dark web🤣🤣🤣
2026-11-13 11:24:07
11
mukhtaar_19
mukhtaar a blacksmith :
we jau
2026-11-14 04:00:45
0
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About