@rashidbattashy: SERIKALI ZANZIBAR YATANGAZA VIWANGO VYA MWENDO BARABARANI ✍🏻 @rashidbattashy Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya marekebisho ya viwango vya mwendo wa vyombo vya moto katika barabara mbalimbali za Zanzibar, ambapo kiwango cha juu cha mwendo katika maeneo ya biashara, skuli, hospitali, Mji Mkongwe na maeneo yenye mikusanyiko ya watu kimewekwa kuwa kilomita 30 kwa saa. Kwa mujibu wa Amri mpya ya Viwango vya Mwendo vya Kitaifa iliyotangazwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, @dr.khalidsalum , marekebisho hayo yamefanyika kwa kuzingatia maoni ya wananchi na wadau wa usafiri kuhusu viwango vya mwendo vilivyokuwa vikitumika. Katika mabadiliko hayo, barabara zote za mitaa zitatakiwa kuzingatia kiwango cha juu cha kilomita 30 kwa saa, huku barabara za ndani zikiwa na kiwango cha juu cha kilomita 60 kwa saa. Aidha, barabara kuu zilizopo ndani ya miji pamoja na zile zinazoingia mijini zitaruhusu mwendo usiozidi kilomita 80 kwa saa, wakati wa mvua kiwango cha juu cha mwendo katika barabara zote za Zanzibar kitakuwa kilomita 30 kwa saa. Serikali imesisitiza kuwa madereva wanapaswa kuzingatia pia alama za barabarani, ambapo endapo bango litaonesha kiwango maalumu cha mwendo, dereva atalazimika kufuata kiwango kilichooneshwa. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha usalama barabarani na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika, ikiwemo kupitia matumizi ya kamera za barabarani zilizoanza kutumika rasmi mwezi Agosti mwaka 2026. Amri hiyo mpya ya viwango vya mwendo inatarajiwa kuanza kutekelezwa rasmi Desemba Mosi, 2026.
Rashid battashy
Region: TZ
Friday 13 November 2026 12:49:25 GMT
Music
Download
Comments
OrTeGa SeMion :
Mabango ya 50kph myatoe sasa
2026-11-13 15:32:41
4
Taxi in Zanzibar- Taxi Company :
kipindi cha mvua unatoka Nungwi mpka Stone Town kwa kilomiter 30 kwa saa. Ifahamike itakua masaa 3 on road [Big LOL][Big LOL]
2026-11-13 16:41:25
0
DIRECTOR ISCO FAKAL :
ongea haraka sina mb
2026-11-13 15:23:11
0
Rosey :
Bora tutembee kwa miguu tu
2026-11-13 14:02:25
0
malik_zein_mohd :
mtupunguzie process za leseni
2026-11-13 15:18:20
1
Suosul :
bado hamjasema Kwanza hizi fain ya mwendo iweje iwe kubwa halafu asie na Leseni ya udereva fain iwe ndogo pinguzeni tozo Zanzibar inchi ya wanyonge mwendo faini sh 233,000 kama mnauza spea
2026-11-13 13:45:52
0
Fadhil.haji :
mchango wangu na mulione hili ili mtumisji wa bara bara au dereva akumbuke basi wekee alama za viwango vya speed kwenye maeneo husika
2026-11-13 14:45:26
1
Maryam Khamis :
na mabango pia baadhi ya sehemu mh Waziri hapana wekeni mfano barabara ya mwera chejuu Na baadhi ya barabr
2026-11-13 13:42:48
1
Othman Hamad :
Mimi hapo kwenye mvua kwaiy kama unatoka nungwi utembe 30 mpk ufike mjini? ama mm sijafamu vizuri?
2026-11-13 14:04:54
1
ZFDC TV :
hilo ndio tatizo la kuzaliwa shamba
2026-11-13 17:23:52
0
LOST :
me pendekezo langu kila palipo n skuli za barabara kuu kuwekwe camera ,kwa maan matuta yanapitwa bila kufatwa sheria,n hivyo t.🤝
2026-11-13 16:19:32
0
King saleh :
Sasa kwa wale walotozwa fain mwanzo
2026-11-13 14:30:19
0
Nofel 🤏😎 :
hi sio Ai
2026-11-13 17:07:53
0
Abdallah aboud :
kwa sote au baazi ya magari
2026-11-13 15:38:19
0
engineering wamichongo :
sasa apo umengea sio 500000000000p😏
2026-11-13 13:35:34
0
Abdul-Malik :
kwahio kama barabara ya cheju - jendele saivi badala ya kutembea 60km watembee 80 au sijaelewa vizuri?
haya sasa kama nihivyo tunaitaji tuone sign barabarani ili mtu likimkuta asijekuleta blaa blaa kama punda na hatakama yupo juu kidogo akiona tu sign mb3le anapata kupunguza na harakati ziendelee bila ya blaa blaa
2026-11-13 15:07:04
0
malik_zein_mohd :
kwa mara ya kwanza hussen mwinyi kunifrahisha ni leo
2026-11-13 15:17:46
1
Rosey :
Muweke alama
2026-11-13 14:07:21
0
Salum salim :
muda wa kutarua sasa😂😂
2026-11-13 15:10:55
0
eddt :
misafara ya viongozi vip au haiwahusu
2026-11-13 15:53:01
0
manga :
Fanyeni mdhibiti na njaa mana kilo moja ya mchele watu wanarekodiwa
2026-11-13 13:24:29
3
Suleimans :
mnapotunga izo sheria mnakua mshakula ama 😃😃😃
2026-11-13 17:05:33
0
Youngmir_2t42 :
duuu angalau kidogo duuu cio aswa
2026-11-13 18:06:23
0
MR.TEDDY🇨🇦 :
vurugu
2026-11-13 14:42:28
0
Meyyan kharusy :
👍👍👍👍
2026-11-13 16:24:46
0
To see more videos from user @rashidbattashy, please go to the Tikwm
homepage.