@jambotv_: VIDEO: Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewatoa hofu na kuwahakikishia mashujaa na wapiganaji wa Vita vya Kagera nchini kuwa watalipwa stahiki zao na pensheni ndani ya mwaka huu wa fedha, kufuatia serikali kukamilisha mabadiliko ya sheria na kanuni zilizokuwa zikikwaza mchakato huo. Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Novemba 13, 2026, mkoani Njombe alipokuwa akisikiliza na kutatua kero pamoja na malalamiko ya wananchi wa Wilaya ya Ludewa. Katika mkutano huo, lalamiko hilo limewasilishwa na Ernest Yohana, mmoja wa wazee wapiganaji wa Vita vya Kagera, aliyezungumza kwa niaba ya wenzake waliofika eneo hilo kutafuta suluhu ya madai yao. Ernest ameeleza kuwa ingawa wanashukuru Serikali ya Awamu ya Siku kwa kuwatambua na kuahidi kuwalipa pensheni, wamekabiliwa na ugumu mkubwa wa maisha kutokana na kuchelewa kwa malipo hayo tangu mwezi Juni mwaka jana. “Tumesubiri tangu mwaka jana mwezi wa sita mpaka sasa kimya. Hilo linatupa shida kwa sababu sasa hivi ni wazee na tunaishi mazingira magumu sana”, ameeleza. Akijibu hoja hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba amekiri uwepo wa madai hayo akifafanua kuwa chanzo kikuu kilichochelewesha malipo hayo kilikuwa ni tofauti zilizokuwepo kati ya sheria na kanuni za wakati walipoandikishwa na sheria za sasa za utoaji wa mafao.
Jambo TV
Region: TZ
Friday 13 November 2026 14:47:59 GMT
Music
Download
Comments
mamy💝💝 :
jamn mavetr mpak Leo wanadai hela zao alf serikal wanakaz ya kuwek bajet ya elninyo😂😂😂😂😂
2026-11-13 18:06:06
27
kichefuchefu :
Kagera ni nchi gani wazee ombi
2026-11-13 17:42:29
2
lujina :
Serikaliii hainaaa helaa saiviii uchumiii wetuuu nimagumu sanaaa kiufupiii
2026-11-14 06:34:55
3
Gidbosta Doughter :
Kama kuna kulipwa mniambie nimwelekeze babangu 😂😂
2026-11-14 16:39:53
6
Justuce Ruhembe :
vipi kuhusu wale walio fariki baada ya vita?
2026-11-13 20:46:05
3
Veronica Msoffe :
na bibi angu alikuwa mgambo alipigana pia
2026-11-20 11:03:49
0
Juwairia Mikidad :
wapeni wazee wetu haki zao
2026-11-13 20:18:35
10
CHIEF MNIMBO :
aeisee mueshimiwa amejibu hili swali vizuri sana
2026-11-13 15:45:34
17
Elias boy :
Hata Mimi Babu yangu alipigana vita ya kagera.
2026-11-13 17:10:04
6
GRAIZER :
Mnajua na cheka nn 😂😂😂
2026-11-15 19:03:46
0
JOSE NGOSHA :
hata mm baba yangu ni viterani wa vita vya kagera
2026-11-13 18:36:53
2
Biker mkiddy :
mambo hayo ni ya kijeshi,
2026-11-13 19:53:30
2
kingi🔹🇹🇿 :
hii inshu Bado tu
2026-11-14 01:45:35
3
Said Haruna :
Mmmmmh!!! Kazi ipoooo
2026-11-13 20:57:53
1
Molley Gabriel :
sawa mzee kowi
2026-11-14 16:08:18
1
Elias samwel :
hii nchi hii
2026-11-14 07:57:32
1
official_july :
ila babu yangu kowi😂
2026-11-14 10:19:03
1
Norah Emmanuel :
mungu akawanguze
2026-11-14 00:29:51
2
BBM437 :
DAAAA ALAFU UNASKIYA BILIONI MIYATATU ZIMEPIGWA DAAA INAUMA SANA
2026-11-13 20:02:21
1
Maua Dar /salasala🌿 :
Mzee wetu nimekuonaaa
2026-11-13 20:58:47
1
jordan :
na mm baba yangu ni veteran wa vita
2026-11-13 19:33:40
1
Jesus Daughter withher grace🥰 :
LUDEWA yetu😢
2026-11-13 21:20:01
1
Dativa Pontion :
Dah
2026-11-13 17:27:17
1
Sanera :
kwahiyo uhuru unadeni
2026-11-13 14:58:08
1
devothakanana :
Mzee anawaka
2026-11-25 11:36:23
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.