@ramsey.natural.he5: FANYA MAMBO HAYA KAMA UNASUMBULIWA NA GESI, KIUNGULIA AU CHOO KIGUMU! Je, unakaa siku mbili au tatu bila kupata haja kubwa? Ukienda chooni unapata shida, unakaza sana au kinyesi kinatoka kwa shida? Au tumbo linajaa gesi na kujaa kila mara? Usizoe hali hii. Choo kigumu cha muda mrefu kinaweza kusababisha au kuchangia kupata bawasiri (hemorrhoids), hasa kutokana na kukaza sana wakati wa kujisaidia. Pia ni muhimu kufahamu chanzo cha tatizo badala ya kulizoea. Jaribu kuanza na mambo haya: 1. Kunywa maji ya kutosha kila siku, hasa asubuhi. 2. Ongeza matunda kama papai, parachichi na mboga za majani. 3. Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi. 4. Fanya mazoezi na usizuie haja kubwa unapojisikia. Kama hali inaendelea kwa muda mrefu, ni vizuri kumuona mtaalamu wa afya ili kujua chanzo chake. Kumbuka: Afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni muhimu. Usisubiri mpaka usumbufu uwe mkubwa. Je, wewe unasumbuliwa zaidi na gesi, kiungulia au choo kigumu? Tuandikie kwenye comment au wasiliana nasi kwa ushauri.#VidondaVyaTumbo #RamseyNaturalHealth #RamseyNaturalHealth #AcidReflux
Ramsey Natural health
Region: TZ
Friday 13 November 2026 17:36:21 GMT
Music
Download
Comments
Bismllah :
matund gn
2026-11-13 18:24:48
0
To see more videos from user @ramsey.natural.he5, please go to the Tikwm
homepage.