@bongodigitaltv_: Kama wewe ni miongoni mwa wale wanaopenda sifa za kuwa wa kwanza kusambaza video za faragha za watu ("connection") kwenye magroup ya WhatsApp au chaneli za Telegram, huu ni wakati wa kufikiria mara mbili kabla hujabonyeza kitufe cha forward. ​Wakili wa kujitegemea, Henry Mwinuka, ametoa tahadhari nzito akibainisha kuwa mchezo huo unaochukuliwa poa mitandaoni unaweza kukugharimu uhuru wako kwa miaka saba jela au kukufanya utoboe mfuko kwa faini ya kuanzia shilingi milioni 20. ​Akipiga stori na AyoTV (@millardayo), Wakili Mwinuka ameweka wazi kuwa wengi hujidanganya kwamba wanakuwa salama kwa sababu si wao waliorekodi video hizo, lakini ukweli wa kisheria uko tofauti kabisa. Ukipokea tu na kuisambaza kwa mwingine, tayari umeshaingia kwenye mtego wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) na EPOCA. ​Kibaya zaidi, hakimu anaweza kuamua kukupa adhabu zote mbili kwa mpigo—yaani ulipe milioni 20 na bado uende jela miaka saba. ​Kwa wale wenye tabia ya kujirekodi wenyewe na kusambaza maudhui yao ya utupu mitandaoni kwa kigezo cha "mwili wangu, maamuzi yangu," Wakili Mwinuka amekata mzizi wa fitina kuwa sheria haikupi kinga hiyo; ukijipost tu umekamatika. ​Mambo yanakuwa mazito zaidi endapo video au picha zinazosambazwa zitawahusisha watoto. Hapo mchezo unabadilika na adhabu inapanda hadi faini ya kuanzia shilingi milioni 50 (au mara tatu ya faida uliyoingiza) na kifungo kisichopungua miaka saba jela. ​Kwa msisitizo huu wa kisheria, ujanja wa mjini sasa ni kufuta maudhui hayo mara tu yanapoingia kwenye simu yako badala ya kuyasambaza, maana sekunde moja ya ku-forward inaweza kubadilisha maisha yako mazima. ​✍🏾 by: @makinizaidi #BongoDigitalTV Bongo Digital TV - #InfoChamber.

BongoDigital TV
BongoDigital TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 13 November 2026 22:21:29 GMT
720
0
0
1

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @bongodigitaltv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About