@millardayo_: Wakili wa kujitegemea, Henry Mwinuka amesema kitendo cha kusambaza picha au video zenye maudhui ya ngono kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp na Telegram, ni kosa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, huku akieleza kuwa Mtu anayepatikana na hatia anaweza kukabiliwa na faini ya kuanzia shilingi milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka saba jela, au adhabu zote mbili. Akizungumza na AyoTV, Wakili Mwinuka amesema zipo Sheria mbalimbali zinazodhibiti vitendo hivyo, ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, pamoja na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), ambazo zinaweka masharti kuhusu usambazaji wa maudhui yasiyofaa kupitia mifumo ya mawasiliano. Ameeleza kuwa Mtu anayepokea video au picha zenye maudhui ya ngono na kuzisambaza kwa Watu wengine anaweza kuwajibishwa kisheria, hata kama si yeye aliyezirekodi, huku akisisitiza kuwa sheria inahusu pia usambazaji wa picha au video za mtu mwenyewe. Aidha, Mwinuka amesema makosa yanayohusisha usambazaji wa maudhui ya kingono ya Watoto yana adhabu kali zaidi, ikiwemo faini isiyopungua shilingi milioni 50 au kiasi kinacholingana na mara tatu ya faida iliyopatikana kutokana na kosa hilo, pamoja na kifungo kisichopungua miaka saba jela. #MillardAyoUPDATES

millardayo
millardayo
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 14 November 2026 00:29:32 GMT
3658
149
10
16

Music

Download

Comments

riahm1237
Riam👑♐️🌵 :
Nishazinguaaa njooniii Mnibebe 😂😂
2026-11-14 01:06:07
0
ole_keiya_001
YEKU S KEIYA🇹🇿🇹🇿 :
mmh kuanzia leo sito omba tena
2026-11-14 00:36:13
1
dullydekey
DULLY DE KEY 🔐 :
mwenye picha mwenyewe anasemaje Na anahukumiajwe nae
2026-11-14 01:20:46
0
abdulimohamedigom
goma mc :
nawanao omba jee wachukuliwe Sheria
2026-11-14 00:41:06
0
reybarbie0
🦚IZ🦋CHELY❤️ :
Samaira mumpe na nyongeza [Tears of joy][Tears of joy]
2026-11-14 01:25:54
0
000glory1
🐅glory💗 :
safiii wamezidi
2026-11-14 00:38:36
0
bobchard728
Bobchard 47@ :
Wana niwuwa yesuuu 😁😁😁
2026-11-14 00:35:31
0
deejay__best
𝗗𝗝 𝗕𝗘𝗦𝗧 :
Amuwez Kunipangia Na UCHI Wangu Full Stop
2026-11-14 00:40:25
2
emmapless
Emmapless⛔ :
Mbona kwenye maelezo hajasema miezi 12 😂, ni Miaka 7 na Milion 20 , kam ni mtu mzima Milioni 50+ kama mtoto 😅
2026-11-14 00:34:30
0
anderssoony
𝐋𝐄𝐄 🕊️ :
Mm kila wapenz wang nawatumia tukikulana kwaiyo nitakaa miez mingap ? Maana sina mpenz mmoja
2026-11-14 01:08:31
0
itsmimah175
Mimahh Henna 😻❣️ :
@Naela🦋💜 😁
2026-11-14 01:18:40
0
ton_gasper
Ton🥇 :
🤣🤣🤣
2026-11-14 00:37:52
0
gbofa17
GB OFA :
🔥🔥🔥
2026-11-14 00:33:08
0
aggynice7
Aggynice :
🥰🥰🥰
2026-11-14 01:18:52
0
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About