@nkingareferralhospital: SIKU YA KISUKARI DUNIANI: ↘️Novemba 14, ni siku ya KISUKARI Duniani, ambapo wadau wa afya Duniani kote huitumia siku hii katika kutoa elimu kwa jamii katika kukabiliana na changamoto hii. - Kaulimbiu ya mwaka huu 2026 inasema, Chukua hatua mapema dhidi ya Kisukari. - Ujumbe huu mkuu unamalengo kadhaa. (i) Kuhamasisha upimaji na ugunduzi wa mapema. (ii) Kutoa elimu kuhusu vihatarishi na dalili za kisukari. (iii) Kuwezesha upatikanaji wa matibabu kwa wakati. (iv) Kuzuia au kupunguza madhara yatokanayo na kisukari. - Hospitali ya Rufaa ya Nkinga tunaendelea kuwashauri wote wanaopata huduma katika taasisi yetu, kuendelea kufuata masharti yote wanayopewa na wataalumu wetu katika matumizi sahihi ya dawa, pamoja na kuwa na mtindo bora wa maisha kwa mustakabali wa afya zenu. - Hospitali ya Rufaa ya Nkinga Tumaini la Afya Yako 🏪 🩺 💊 💉 #hospital #doctor #health #tabora #tiktoktanzania🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Nkinga Referral Hospital
Nkinga Referral Hospital
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 14 November 2026 10:04:25 GMT
59
2
0
1

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @nkingareferralhospital, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About