@zoomonlinetv2: Mzozo umeibuka katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kibaha kati ya Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyversta Koka, na Meya wa Manispaa hiyo, Dkt. Nicas Mawazo, ambaye ndiye Mwenyekiti wa kikao. Katika tukio hilo lililotokea Novemba 13, 2026, Mbunge Kona alisimama na kuanza kuzungumza bila kupata ruhusa ya Mwenyekiti. Alipoelekezwa kukaa chini, aligoma kutekeleza maelekezo hayo na kuendelea kusisitiza apewe nafasi ya kuzungumza. Katika malumbano hayo, Meya alimuhoji Mbunge Koka kuhusu kuingia kwenye kikao cha baraza bila kuvaa joho, akirejea kanuni za baraza zinazohusu mavazi rasmi katika vikao hivyo. Akijibu hoja hiyo, Kona alidai kuwa tayari alikuwa ameliandikia barua chama chake kuhusu suala la kuvaa joho katika vikao vya madiwani, akieleza kuwa alikuwa amelifikisha suala hilo kwa chama. Hata hivyo, hali hiyo ilizua malumbano kati yake na Meya, huku Mbunge huyo akisisitiza haki yake ya kuzungumza kama mwakilishi wa Jimbo la Kibaha Mjini na kupinga namna Mwenyekiti alivyokuwa akiendesha kikao. #MzalendoTvUpdate
Zoom online Tv
Region: TZ
Saturday 14 November 2026 15:59:39 GMT
Music
Download
Comments
julius :
The MP is arrogant
2026-11-14 17:30:18
9
user762048536540 :
Mruhusu mbunge wetu aongee mbona unamyanyasa mkombozi wetu koka? By F msechu
2026-11-14 17:23:57
8
Method Oscar :
mbunge namwelewa vizuri sana hao madiwani wana dharau sana
2026-11-14 18:18:19
9
King P :
uzuri wanapambana ccm A na ccm B
2026-11-14 17:50:44
11
👌 :
MP wa kibaha ametawala muda mrefu sana aondoke analeta mazoea sasa
2026-11-14 17:51:20
4
robin :
hapana watu wanafikia kutoeshimiana c kitu kizuri huyu ni mueshimiwa mbnge ana heshima yake na wakuu wengine kama dc mkuu wa mkoa na watu wengine wafikie kuheshimiana ili mkoa wetu mchanga uendelee na c malumbano
2026-11-14 18:59:01
2
msafirimwambela71 :
ikiona hvyo wamezurumiana pesa za diri
2026-11-14 17:40:30
6
Dr Ahmed Mmanga :
Sasa endeleeni kushulikiana wenyewe kwa wenyewe sasa Chama kimoja
2026-11-14 19:11:48
2
Rashidi Mashaka :
Teali kumesha Anza kuchangamka Sasa.
2026-11-14 18:39:33
2
Shenye Lugiko :
mabaraza mengi yanakumbwa na hali ya kutoelewana kati ya m/kiti na mbunge wake kisa siasa huwa haziishi
2026-11-14 17:48:07
3
emanuelimushi290 :
safisana. komaa. wasikuburuze.
2026-11-14 20:23:40
1
Shebby :
shida wazaw wa kibaha.yani wazaramo wanawaachia wageni wanaongoza wanaleta marumbano.wamevimbilwa
2026-11-14 19:45:21
1
J,brand :
sio dharau Hawa nd watu tunao watak yy hataki kuendeshwaa
2026-11-14 17:58:04
0
Saimoni Kushoka :
mimi naitwa. kushoka nawaomba msigombani
2026-11-14 18:05:48
0
Missy💐 :
heheheh
2026-11-14 17:54:28
0
mwal Ndabise :
Huyu mbunge wa chama gani
2026-11-14 18:11:36
2
zakayo :
Hii ni mifumo mibovu ya kiutawala mara DC naye ni sehemu ya kikazi cha madiwani,
2026-11-14 17:57:39
2
Adrian :
Nilihitaji kukutetea, but upo kwaajili ya chama sio km muwakilishi wa wananchi kaa kmya
2026-11-14 18:09:32
1
edwardkimangila :
Kumeanza kuchangamka huku kwetu
2026-11-14 17:15:53
1
Benard Otuoma :
Naomba Mungu hawa ccm wavurugane kwenye hicho chama mpaka chama kipasuke, kuanzia juu mpaka chini
2026-11-14 19:33:54
0
GASPER KISINZA :
KWANIN BARAZA LISIMCHUKULIE HATUA?
2026-11-14 20:24:03
0
abuumakele :
mbunge kaongea vizuri kabisa kuna watu wanazalau wakipata kiti😁😁
2026-11-14 20:22:13
0
coltildampemba :
Nchi ngumu sana hii 💔🇹🇿
2026-11-14 19:54:00
0
Steve white :
uzuri wote ni familia, chama kimoja lakn hawaelewani
2026-11-14 21:20:57
0
Victor Mraha :
Ila Kuna baadhi ya viongozi ujiona MUNGU pindi wanapokuwa kwenye nafasi fulani Upuuzi mtupu.Ila haya maisha bhna hamna mwenye hitimisho la mwisho mbele ya mwanadamu
2026-11-14 17:40:14
0
To see more videos from user @zoomonlinetv2, please go to the Tikwm
homepage.