@ngasatvdodoma: TAKUKURU WAAGIZWA KUCHUKUA HATUA MRADI WA TACTIC LINDI. *📌 Mkandarasi Ashikiliwa na Jeshi la Polisi* Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)na Jeshi la Polisi kuchunguza matumizi ya fedha za mradi wa kuboresha miundombinu ya Manispaa ya Lindi, baada ya taarifa kuonesha kuwa mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 4.22, lakini utekelezaji umefikia asilimia 24 pekee huku asilimia 80 ya muda wa mkataba ikiwa imetumika. Akitoa maelekezo hayo leo wakati wa ziara yake mkoani Lindi, Makamu wa Rais ametaka kufahamishwa namna malipo yalivyofanyika, fedha zilivyotumika na sababu za kazi kutotekelezwa kwa kasi iliyotarajiwa. Pia ametaka taarifa ya uchunguzi imfikie yeye mwenyewe ili aiwasilishe kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.