@almecky_tz: Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA) limetuma salamu maalum za pongezi kwa Zanzibar kufuatia uzinduzi wa maono makubwa ya Zanzibar Astronomy and Space Society (ZASS) pamoja na ujenzi wa Zanzibar Space Observatory na Planetarium. Kupitia ujumbe wa video uliowasilishwa katika hafla hiyo, Casey Swails, Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa NASA amesema kuwa licha ya kushindwa kuhudhuria hafla hiyo ana kwa ana, anajisikia heshima kubwa kushiriki sherehe hizo kwa njia ya mtandao. Swails amewapongeza wote waliofanikisha mradi huo, akisisitiza kuwa Observatory na Planetarium si majengo na darubini pekee, bali ni fursa kubwa kwa maendeleo ya elimu, utafiti na ugunduzi wa kisayansi. "Mnajenga sehemu ambapo mwanafunzi ataangalia kupitia darubini kwa mara ya kwanza na kugundua kuna ulimwengu mzima unaomsubiri kuchunguzwa. Mnajenga fursa kwa walimu, watafiti na wahandisi wa baadaye, na sehemu ambapo udadisi unaweza kukua na kuwa uwezo." amesema Swails. Aidha, amemshukuru Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuunga mkono mradi huo na uongozi wake katika kuhakikisha maono hayo yanageuka kuwa uhalisia. Akizungumzia mustakabali wa shughuli za anga za juu, Swails amesema NASA kwa sasa ipo katika kipindi cha kusisimua kupitia mpango wa Artemis, wenye lengo la kuwarudisha binadamu Mwezini na kujenga msingi wa kudumu huko, ikiwa ni hatua ya kuelekea Mars na maeneo mengine ya mbali zaidi. Ameongeza kuwa safari hiyo haiwezi kufanikishwa na nchi moja pekee, bali inahitaji ushirikiano wa watu na taasisi mbalimbali duniani. "Ugunduzi daima umekuwa ni mchezo wa timu. Unahitaji walimu, wanasayansi, wahandisi, sekta binafsi na jamii zote kufanya kazi pamoja. Ndiyo maana mashirika kama ZASS ni muhimu. Mustakabali wa anga hautaundwa na nchi moja au taasisi moja tu, utaundwa na watu duniani kote waliohamasishwa kuchunguza, kugundua na kuchangia." amesema. Amehitimisha kwa kusema kuwa kile kinachojengwa Zanzibar ni sehemu ya mustakabali huo, kupitia uwekezaji katika vipaji, elimu na wazo kwamba kizazi kijacho cha wagunduzi kinaweza kutoka sehemu yoyote duniani. #Zanzibar #Tanzania #Habari #Football #Trending
almecky_tz
Region: TZ
Sunday 15 November 2026 08:29:48 GMT
Music
Download
Comments
Keys :
Congratulations 🥳 Zanzibar and our beloved President Ali Hassan Mwinyi
2026-11-15 09:30:10
0
iSmile :
Zanzibar gani??
2026-11-15 09:26:40
0
عبد الله بن مولد. 🇦🇪🇹🇿 :
Uyoo ndo Mwinyi 💯
2026-11-15 09:50:29
0
Mufti :
2026-11-15 09:08:06
0
To see more videos from user @almecky_tz, please go to the Tikwm
homepage.