@safe.agrochemical: Acha kununua mbolea kwa kufuata mkumbo au jina lake maarufu tu! 🚫🌱 Kufanya hivyo kunaweza kukuletea hasara ya pesa na mavuno hafifu. Kila mbolea ina kazi yake maalum shambani: 🔹 DAP: Hii ni ya kupandia. Inasaidia mmea kuota na kushika mizizi imara. 🔹 CAN & Urea: Hizi ni za kukuzia. Zina naitrojeni nyingi ya kunawirisha mmea. 🔹 NPK: Usiangalie jina tu! Angalia namba za uwiano kwenye mfuko kulingana na mahitaji ya zao lako. Kumbuka: Kuweka mbolea nyingi siyo siri ya kuvuna sana. Ukiweka kupita kiasi au nje ya muda, unaunguza mazao na kupoteza mtaji. 💸 Jua udongo wako, jua zao lako. Kwa mafunzo zaidi ya kilimo bora na matumizi sahihi ya mbolea, fuatilia SAFE AGROCHEMICALS 👇 #KilimoBiashara #MboleaBora #KilimoChaKisasa #safeagrochemical