@mr.niga06: Wakili wa kujitegemea, Henry Mwinuka amesema kitendo cha kusambaza picha au video zenye maudhui ya ngono kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp na Telegram, ni kosa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, huku akieleza kuwa Mtu anayepatikana na hatia anaweza kukabiliwa na faini ya kuanzia shilingi milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka saba jela, au adhabu zote mbili. Akizungumza na AyoTV, Wakili Mwinuka amesema zipo Sheria mbalimbali zinazodhibiti vitendo hivyo, ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, pamoja na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), ambazo zinaweka masharti kuhusu usambazaji wa maudhui yasiyofaa kupitia mifumo ya mawasiliano. Ameeleza kuwa Mtu anayepokea video au picha zenye maudhui ya ngono na kuzisambaza kwa Watu wengine anaweza kuwajibishwa kisheria, hata kama si yeye aliyezirekodi, huku akisisitiza kuwa sheria inahusu pia usambazaji wa picha au video za mtu mwenyewe. Aidha, Mwinuka amesema makosa yanayohusisha usambazaji wa maudhui ya kingono ya Watoto yana adhabu kali zaidi, ikiwemo faini isiyopungua shilingi milioni 50 au kiasi kinacholingana na mara tatu ya faida iliyopatikana kutokana na kosa hilo, pamoja na kifungo kisichopungua miaka saba jela. #millardayoupdates

Turo-Niga06
Turo-Niga06
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 15 November 2026 15:59:45 GMT
1386
7
1
0

Music

Download

Comments

binti.kigoma3
Baby jayper :
Nipo tayar kwenda jelaa msosi si uhakikaaaa au😂😂😂
2026-11-15 18:01:44
0
To see more videos from user @mr.niga06, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About