@alexphilimon2: RUKWA: SOKOMATOLA YAZUA MVUTANO SUMBAWANGA, MADEREVA WASITISHA HUDUMA BAADA YA UHAMISHO WA STENDI Huduma za usafiri wa umma na shughuli za kibiashara katika Manispaa ya Sumbawanga zimekumbwa na sintofahamu kufuatia uamuzi wa uongozi wa Manispaa kuhamisha kituo cha zamani cha mabasi cha Sokomatola na kuelekeza watumiaji wa kituo hicho kwenda Stendi Kuu ya Katumba na Kanondo. Hatua hiyo, inayolenga kupanga upya shughuli za usafiri na kuboresha miundombinu ya mji, imeibua malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wadogo (Machinga), abiria na madereva wa vyombo vya usafiri ambao wameathirika na mabadiliko hayo. Wakizungumza katika eneo la Sokomatola, Mwenyekiti wa Stendi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wamesema kuwa walikuwa na taarifa za awali kuhusu mpango wa kuhamishwa, lakini changamoto kubwa iliyopo ni mazingira na utaratibu wa utoaji huduma katika maeneo mapya waliyoelekezwa. Hali imezidi kuwa ngumu baada ya madereva wa magari ya abiria kusitisha huduma za usafiri, wakieleza kutoridhishwa na kukosekana kwa utaratibu utakaowezesha usafiri wa uhakika kati ya vituo vipya na maeneo ya katikati ya mji. Kutokana na hali hiyo, wananchi wanaotegemea usafiri huo kwa shughuli zao za kila siku wamejikuta katika wakati mgumu, huku shughuli za biashara katika eneo hilo nazo zikikumbwa na changamoto. Wananchi na wadau wa usafiri wameiomba Manispaa ya Sumbawanga kuingilia kati na kutoa ufafanuzi kuhusu mgawanyo wa vituo hivyo. Wamesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa utaratibu ulio wazi, wakibainisha kuwa Stendi ya Katumba imejengwa kwa ajili ya mabasi ya mikoani, hivyo wanahitaji kufahamu eneo rasmi litakalotumika kama stendi ya mabasi ya ndani na yale yanayohudumia wilaya jirani. Wadau hao wanaamini kuwa kuwepo kwa suluhisho la pamoja kutasaidia kurejesha huduma za usafiri, kulinda shughuli za kiuchumi na kupunguza usumbufu kwa wananchi. Hadi sasa, wananchi na wadau wa usafiri wanasubiri hatua na ufafanuzi wa uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga ili kumaliza changamoto hiyo na kurejesha hali ya kawaida ya usafiri na biashara mjini humo. HABARI ZA RUKWA NA MATUKIO MBALIMBALI, ENDELEA KUFUATILIA. #Rukwa #Sumbawanga #Sokomatola #Habari
Alex Philimon
Region: TZ
Tuesday 17 November 2026 08:49:45 GMT
Music
Download
Comments
Ibrahim jamsoni :
kwani uyo mkuu wa mkowa rukwa ninani🤔
2026-11-17 11:49:10
3
568299 :
Nayo Sumbawanga Haina msimamo,kipondi kile walisema wahamie katumba mara wakarudisha Tena stand ya zamani yaani wavutane tu sisi tupo tunasubiri msimamo wao
2026-11-17 09:44:29
3
MNYAMA THE DON :
Na ndomana kuna stendi ku katumba shida ya wanasoko matola uwlewa ni mdogo
2026-11-17 16:29:56
1
Gianna in 🇰🇪 :
jmn kaka anguh masumbuko😳
2026-11-17 10:39:42
1
Pink🌸 :
Pia kanondo mzunguko wa hela ni mdogo sana jamn watu watateseka sasa mtu aende kanindo na anamtaji wa ef10 nauli kwenda na kurud ef 2 aisee hali ni mbaya
2026-11-17 14:42:51
0
linh sang :
nimemuerew huyo dad
2026-11-18 17:32:29
0
Binti makaza :
felista.
2026-11-18 08:49:02
1
Flavy Daud :
Uwiiiiiiih 🙌 nirudi Sasa katumba home sweet homie pachangamke akiiiiii
2026-11-18 14:06:44
0
Abubakr :
mwenyekiti mnae
2026-11-18 14:33:32
0
GM :
naomba tu selikali isiruhusu vikao Wacha pachangamke tuuuu
2026-11-18 04:58:04
1
kassanu :
Katumba stendi aifanyi kaziau
2026-11-17 14:11:59
0
nurath 😋💘 :
duuuu kweliii noma polen
2026-11-17 09:12:04
0
Kansapa :
kukosa msimamo
2026-11-17 10:29:17
0
Bonge la Bwana :
maelekezooooo
2026-11-17 17:05:46
0
Sarah Kasunga :
duuuh tupo apa apa atujuwiiiii kinacho endeleaa
2026-11-17 13:54:17
0
Jackline🇹🇿 :
duuh
2026-11-17 13:58:11
0
Gress Kazembe :
waende katumba
2026-11-17 14:02:03
1
MR ISSAH :
selikali nayo iache mamb ya hovyo bwama ee
2026-11-17 12:19:37
1
Hilda :
wan wanyanyas san
2026-11-18 08:01:53
0
Asia William :
Mweeeeeee kaka angu masumbuko posutaa taaa mweeeeee zyamanda mweee 😅
2026-11-18 12:18:14
0
Elisterrryhhh :
waenda katumba
2026-11-17 20:04:04
0
manyota mc :
vitakamilika mkiwa huko bwana wanateseka wapi wewe
2026-11-17 20:04:13
0
Sophia Alex :
ila jaman bac2 iv kwan awaoni kama galama ni kubwa sana yan adi ufike kanondo ni garama sana
2026-11-18 18:41:15
0
Gress siliveli :
ndomana kanondo nistendi ndogo itasaidiana nakatumba
2026-11-17 19:33:39
0
Steve to boy :
Njonenikatumba msisumbuwe
selekali
njonene
katumba aukanondo
2026-11-17 10:59:23
1
To see more videos from user @alexphilimon2, please go to the Tikwm
homepage.