@jamvilahabari: Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka viongozi kuacha malumbano na migogoro isiyo na tija, akisisitiza kuwa uongozi haupimwi kwa uwezo wa kugombana na wengine, bali kwa namna viongozi wanavyoshirikiana kuwaletea wananchi maendeleo. Amesema tabia ya viongozi kutofautiana na kushughulikia migogoro badala ya kushirikiana inakwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika halmashauri na taifa kwa ujumla, huku wananchi wakiendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Amewataka viongozi kuelekeza nguvu zao katika mambo yenye manufaa kwa wananchi, ikiwemo ubunifu, ushirikiano na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika malumbano. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutokea mvutano kati ya Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylvester Koka, na Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Novemba 13, 2026, kufuatia kutofautiana kuhusu utaratibu wa uendeshaji wa kikao hicho. #jamvilahabaridigital
jamvilahabari
Region: TZ
Tuesday 17 November 2026 19:45:49 GMT
Music
Download
Comments
Yilod Hasunga :
shughulika naooo
2026-11-17 22:25:21
1
user5135066882233 :
Huyo mbunge hatoshelizi mwnye mamlaka ni meya
2026-11-18 08:54:09
0
Jakobo Madanda :
kila...mmoja...ana...haki....sawa..ya..kusikilizwa...sio....dhamana...wala...cheo...kitutenge....na...wananchi...hapana.....
nilikuwa...naomba...tutoe...umimi...hata...kwenge...matukio...ya...kiserikali..kijamii...na...kisiasa...sate...tuwe...sawa
2026-11-18 16:25:42
0
Phoebe Mshana :
Vitu vya aibu sana kiukweli
2026-11-18 10:23:48
0
Phoebe Mshana :
Hapo Kuna shida kubwa sana kwenye wilaya yetu ya Kibaha! hapo hakuna kuelewana kabisa
2026-11-18 10:24:41
0
Ally Mkwaju :
ngera sana mkuu haikuleta picha nzur
2026-11-18 06:56:49
0
To see more videos from user @jamvilahabari, please go to the Tikwm
homepage.