@suluhisho_lauzazi1: Dada yangu, kama umekutana na mwenza wako na sasa unasubiri kujua kama ujauzito umetokea, usiwe na haraka ya kupima! Kuna jambo muhimu unapaswa kulijua: Siku 1–5 baada ya tendo: Ni mapema sana, kipimo hakiwezi kuthibitisha ujauzito. Siku 6–10: Yai lililorutubishwa linaweza kuwa linaanza kujipandikiza kwenye ukuta wa kizazi, lakini bado ni mapema kwa kipimo cha mkojo. Siku 10–14: Baadhi ya vipimo nyeti vinaweza kuanza kusoma ujauzito. Baada ya kukosa hedhi: Huu ndio muda unaoshauriwa zaidi kupima kwa kipimo cha mkojo. ❤️ Ushauri wangu: Pima kuanzia siku ya kwanza unapokosa hedhi. Kama majibu ni negative lakini hedhi haijaja, rudia baada ya siku 2–3. Kumbuka, kupima mapema sana kunaweza kukupa majibu hasi wakati ujauzito upo lakini homoni ya hCG bado haijafikia kiwango cha kusomeka. SWALI: Wewe huwa unapima mimba baada ya siku ngapi tangu kukutana na mwenza wako? Andika kwenye comment tujifunze pamoja. #AfyaYaUzazi #KipimoChaMimba #Ujauzito #SafariYaUzazi #DrDickson