@uhuruonline: #HABARI : MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kutoa kipindi cha miezi mitatu kabla ya kusitisha matumizi ya Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) pekee kwa wananchi ambao tayari wamepatiwa vitambulisho. Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, Toleo la 2026, akiwataka wananchi wenye namba pekee kujitokeza kuchukua vitambulisho vyao. Ameeleza kuwa wapo wananchi waliosajiliwa na kupata namba za utambulisho lakini hawajachukua vitambulisho vyao, hivyo amewataka kutumia kipindi hicho kuhakikisha wanavipata kabla ya muda uliotangazwa kumalizika. Aidha, Kaji amesema NIDA itaanza kutoa vitambulisho vipya kwa wananchi waliosajiliwa lakini hawajavipata, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kufuatilia taarifa na maelekezo yanayotolewa na mamlaka hiyo. #uhuruonline #uhuruupdates

uhuruonlinetz_
uhuruonlinetz_
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 18 November 2026 11:03:19 GMT
248437
12629
882
1465

Music

Download

Comments

2025sameza
SMZ. :
tunavipata wap wakati mnatuzungusha wakuu hiii nchi jamani khaaa
2026-11-18 19:16:12
271
cleverzacharia8
clever Zacharia :
Vitambulisho tumien nyie maana tukienda Mnasema havipo
2026-11-18 22:17:13
150
bilalwilliam2
king Bilal :
FUTENI TU TULISHAZOEA
2026-11-19 06:15:02
39
hawaayubu80
hawaayubu80 :
namm niliko mbali njee yanchi Zanzibar [Laugh approved][Laugh approved]
2026-11-19 11:48:01
0
moreensanga4
maria :
Kumekucha [Big LOL][Big LOL][Big LOL][Big LOL]
2026-11-19 11:35:27
0
neyblessed3
ney blessed :
yanii mlisema tutapata msg ya kwamb kitambulisho kimetoka lakin toka mwaka jana akuna msg tutajuaj
2026-11-19 03:50:01
37
user7754304625215
Sanga🌺 :
nacc ambao hatuna nida Wala kad ya mpiga kula Wala chet Cha kuzaliwa,,,mnatusaidia
2026-11-19 11:15:17
11
brown.gerald
brown gerald :
kilaaa nikienda naambiwa nasubili meseji
2026-11-19 05:42:52
10
khadija.juma168
Khadija🇴🇲🥰🇹🇿🥰 :
tulioko nje ya nch jmn tunafanyeje
2026-11-19 08:27:50
10
l.....e16
my corazòn🤗⚡ :
stishen wala atutishi[Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-11-19 07:16:12
0
gracesimba1
Gee🔐🦋🦋 :
mm nasubili mpaka leo mesej ya kufata lkn sija tumiwa
2026-11-19 13:19:08
6
zainabu.aljabiri
Zainabu Aljabiri :
jamani wengine tupo omani jaman tufanyeje
2026-11-19 06:19:47
14
itsjames250
James 🍁 :
mbn tunatishana kingese
2026-11-19 09:33:31
0
imma.malley7924
malley meta :
sasa tutachukulia wap maana tumeambiwa mtapewa taarifa had leo sijapata taarifa yeyote
2026-11-19 09:10:59
6
sashamoney4
ساشا موني🌺 :
mtumeeee nimeisha[Tears of joy]
2026-11-19 07:58:38
0
anna.potami
Anna Potami :
vitambulisho vyenyewe vinafutika kama vina ukoma bhana futeni tu
2026-11-19 11:29:21
6
m4350123
🦋M :
Yaan tuliambiwa msg zitatumwa za kwenda kuchukua vitamburisho mpk sah msg haijawah kutumwa harafu et wanafuta 😳
2026-11-18 20:40:27
19
aazah066
A'azah066 :
Nina mwaka sasa kila Siku nafanya KAZI ya kwenda NIDA kufata kitambulisho naambiwa bado nisubiri toka 2025 mpk Leo ,Alf nauli sio chini ya 6k kwenda na kurudi,aanh vyovyote vile bhn mi sirudi saiz
2026-11-19 12:01:24
2
its.chduke
it's chduke😜 :
UKIENDA UNAAMBIWA HAVIJATOKA😁
2026-11-19 03:27:51
10
tiktokio284
SNOW :
mwenzetu uko dunia ganiii!!? leo tarehe 19?
2026-11-18 14:37:38
8
happiness.nessi
Happiness Nessi :
yaani mm sina wala sijawahi kwenda kujiandikisha kbisa
2026-11-19 07:27:33
0
ndilla0743
mboga..7% :
tuleteen nyumban wakuu ikiwapendeza alaf ustufokee.. tukija wenyew ofisin kwenu mizunguko mingi sasa tuwaelewe vp
2026-11-19 13:40:42
1
aso.mtu.ana.mungu3
husna :
Sisi wengine tuko dubai na kumtuma mtu haiwezekani tunafanyaje
2026-11-19 12:27:29
1
prisca32211
prisca32211 :
Namm niliyepoteza je
2026-11-19 10:24:20
0
olubi.123
Olubi @123 :
fanyeni utaratibu tupokea popote kadi badala ya sehemu au mkoa uliojiandikisha
2026-11-19 10:25:52
0
To see more videos from user @uhuruonline, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About