@matumla.boxing.promotion: TAARIFA YA USHIRIKI WA MSIBA – MATUMLA BOXING PROMOTION Matumla Boxing Promotion inapenda kutoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba wa kuondokewa na mpendwa wetu Mzee Habibu Kinyogoli. Uongozi wa Matumla Boxing Promotion ulikuwa sehemu ya msiba huu na kushiriki katika shughuli zote za msiba kuanzia mwanzo hadi mwisho, ikiwa ni ishara ya upendo, mshikamano na kuthamini mahusiano mema ndani ya jamii ya ngumi na nje ya jamii hiyo. Shughuli za msiba zilifanyika Gongo la Mboto, Kituo Kipya, huku mazishi yakifanyika Mwanalumango, Kisarawe. Tunatoa pole kwa familia nzima na wote walioguswa na msiba huu. Katika kipindi hiki kigumu, tunawaombea subira, nguvu na faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Innalillahi wa inna ilayhi raji'un. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Habibu Kinyogoli mahali pema peponi. Amina. MATUMLA BOXING PROMOTION Umoja, Upendo na Mshikamano. #tiktoktanzania🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #ugandatiktok🇺🇬 #habibukinyogoli #boxing🥊
Matumla Boxing Promotion 🥊
Region: TZ
Wednesday 18 November 2026 13:02:48 GMT
Music
Download
Comments
mrs j .. :
mung amlaz maali pema pepon
2026-11-18 19:23:07
0
Team lete kaz tufanye kaz :
tuta mkumbuka milele coach kinyogor
2026-11-18 19:12:15
0
Matumla Boxing Promotion 🥊 :
2026-11-18 13:07:01
1
sidebare :
inalilah waina ilayh rajiuun
2026-11-18 18:41:56
0
To see more videos from user @matumla.boxing.promotion, please go to the Tikwm
homepage.