@binotv03: Meli ya MV Mwanza yanusurika kugongana na Kivuko cha abiria Meli ya MV Mwanza imegonga mwamba wa Bismarck (Bismarck Rock) katika Ziwa Victoria, jijini Mwanza, leo Jumatano majira ya saa 4:30 asubuhi, ikiwa imebeba wadau wa sekta ya uchukuzi waliokuwa kwenye ziara ya kutembelea ziwa hilo. Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea wakati meli hiyo ilipokuwa katika hatari ya kugongana na kivuko cha abiria kilichokuwa kikitokea Sengerema, hali iliyosababisha meli hiyo kugonga mwamba wakati wa kujaribu kuepusha ajali. Aidha, taarifa za awali zinaeleza kuwa hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa kwa abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo. Wadau hao wa sekta ya uchukuzi walikuwa jijini Mwanza kuhudhuria Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (Joint Transport Sector Review Meeting).

BINO TV 🎙️🎙️
BINO TV 🎙️🎙️
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 18 November 2026 16:32:42 GMT
4469
110
4
1

Music

Download

Comments

sidleymalege45
sidley malege :
mbna unaonesha meli nyingne na wakati ni ile kubwa we vp mbna mnataka kutuchanganya
2026-11-18 20:41:54
0
jackison253
Sangwa fetines :
[Like][Like][Like]
2026-11-18 19:44:05
0
To see more videos from user @binotv03, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About