@popularmedia_tz: Kitambulisho cha Taifa cha NIDA kinatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya taratibu za kufunga ndoa nchini, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha wahusika wanatambulika rasmi na kuzuia wageni kujifanya Watanzania kupitia ndoa ili kupata utambulisho wa uraia. Akizungumza katika uzinduzi wa kitambulisho kipya cha Taifa toleo la 2026, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema tayari wamezungumza na viongozi wa dini kuhusu utaratibu huo, akisisitiza kuwa mtu asiye na kitambulisho cha NIDA hataruhusiwa kufunga ndoa. Ameongeza kuwa mifumo ya NIDA itaunganishwa na huduma za usajili wa vizazi, ndoa, talaka na vifo ili taarifa hizo zipatikane na kusimamiwa katika mfumo mmoja, ikiwa ni sehemu ya safari ya kujenga Tanzania ya kidijitali. #habari #habari_zinazo_trending #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #tanzania
Popular Media_Tz
Region: TZ
Wednesday 18 November 2026 17:06:37 GMT
Music
Download
Comments
mzaramo :
ndoa gani
2026-11-18 18:52:33
0
Denisi Mvanda :
🥰🥰🥰
2026-11-18 17:16:05
0
To see more videos from user @popularmedia_tz, please go to the Tikwm
homepage.