@tangavision1: TANGA YAENDELEA KUPIGA HATUA! PROF. SHEMDOE AIPONGEZA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA TACTIC. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga chini ya Mstahiki Meya, Mhe. Seleboos Mustafa, pamoja na Mkurugenzi wa Jiji, Bw. Philemon Mwita Magesa, kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TACTIC). Pongezi hizo zimetolewa Novemba 18, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa jijini Tanga. Katika ziara hiyo, Prof. Shemdoe ametembelea miradi ikiwemo ujenzi wa Ofisi za Uhandisi, ujenzi wa barabara, Soko la Makorora pamoja na ujenzi na uboreshaji wa fukwe za Raskazone. Ameeleza kuridhishwa na kasi na mabadiliko makubwa yaliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ndani ya kipindi kifupi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia miradi ili ikamilike kwa viwango vinavyotakiwa. Kwa mujibu wa taarifa hiyo,miradi hiyo inatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 28, 2027, na kuanza kutoa huduma kwa wananchi. Tanga inaendelea kubadilika kupitia uwekezaji katika miundombinu, huduma za kijamii na mazingira ya biashara na utalii. #TangaVision #TangaDevelopment #TACTIC #TangaCity #MaendeleoYaTanga

Tanga Vision
Tanga Vision
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 18 November 2026 17:25:24 GMT
4003
144
6
11

Music

Download

Comments

gpgo033
👌 :
Titaona shasha
2026-11-18 19:58:33
1
user2728670258781
dondo :
wagosi tupo
2026-11-18 18:16:45
3
yaumu.juma
Yaumu Juma :
ebu tutengenezeeni barabara yalushoto mlalo mbwana tumechoka kuwaomba
2026-11-18 18:43:20
1
muya.snr
Muya Snr :
Rais katoa au mkopo! Pesa ya wafadhili hiyo[Laugh approved][Laugh approved]
2026-11-18 18:51:00
1
khai.khais
Khai Khais :
[Like][Like][Like]
2026-11-18 18:48:08
1
To see more videos from user @tangavision1, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About