@sautiyanjombe: 🇹🇿 NIDA YAZINDUA VITAMBULISHO VIPYA VYA TAIFA VYENYE TEKNOLOJIA YA KISASA! Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. James Kaji, ameeleza maboresho makubwa yaliyofanyika katika Kitambulisho cha Taifa toleo jipya la mwaka 2026. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitambulisho hicho uliofanyika Novemba 18, 2026, Kibaha mkoani Pwani, Dkt. Kaji amesema maboresho hayo yamelenga kuimarisha usalama, kuongeza uimara wa vitambulisho na kupanua wigo wa huduma zinazoweza kupatikana kupitia kitambulisho kimoja. Amefafanua kuwa teknolojia ya Laser Engraving itatumika kuchonga taarifa na picha za mwananchi ndani ya tabaka la kitambulisho ili kuzuia kufutika kwa maandishi na picha. Pia, kadi mpya zimeongezewa QR Code na Machine Readable Zone (MRZ) kwa ajili ya kurahisisha uhakiki wa taarifa. Aidha, nafasi za kuunganisha huduma za kidijitali zimeongezeka kutoka nne hadi nane, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kama bima ya afya, taarifa za vyeti vya kuzaliwa, TIN na leseni za udereva. Kwa upande mwingine, Serikali imefafanua kuwa vitambulisho vya zamani bado vinaendelea kutambulika na kutumika, hivyo wananchi wenye vitambulisho vilivyo katika hali nzuri hawalazimiki kuvibadilisha kwa sasa. Je, una maoni gani kuhusu maboresho haya ya Kitambulisho cha Taifa? #NIDA #VitambulishoVyaTaifa #Tanzania #Teknolojia #HabariLeo

SautiYaNjombe
SautiYaNjombe
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 19 November 2026 12:49:29 GMT
48787
1775
242
291

Music

Download

Comments

veemoney_1
VEEMONEY :
Naona jua lina changanya watu[Tears of joy]
2026-11-19 19:27:53
24
mwajumamichael87
mwajuma_ :
Sawaa no problem 😂😂😂
2026-11-19 22:09:41
0
majayden62
@cute :
[Laugh approved][Laugh approved] nmekosa vyote sio ndoa wala nida nitaishia kuwa mchepuko
2026-11-20 02:47:20
1
user2105298885817
Missing my mum :
[Laugh approved][Laugh approved][Laugh approved][Laugh approved] kwani lazima kuolewa mnataka tu kutuchosha
2026-11-19 21:23:12
1
modester.agai
Modester Agai :
😁😁😁😁😁😁 ila bongoooo
2026-11-19 23:04:21
0
tinaa13906
tinaa :
naomb kujua nida ni msaidizi wa ndoa ama ni nin??
2026-11-19 20:20:14
6
graceteddie560
Njombe Sweet cake 🎂 :
sindio
2026-11-20 05:07:00
0
justinagwello
RenePrecious :
eeeh ngoja nitafute nida kwanz 😂😂😂
2026-11-20 00:46:04
0
user4346696025095
Devotapatrick01@ :
kwaiyo tuliofunga NDOA bila NIDA inakuwaje
2026-11-19 18:03:52
0
da.naj.tz
Da naj tz :
uzuli Sina iyo NIDA Wala iyoo ndowa sitaki na nikifa mtajuwa wenyewe
2026-11-19 21:50:24
0
katoto723
katoto :
kwan nimewambia naenda kuolewa na hy nida jaman
2026-11-19 20:05:14
0
user27480017913548
D ns♥️ Celina :
Sasa mfano Mimi simjuw hata mama angu Alie ni zaa vip kuhusu cheti napata wapi sasa
2026-11-19 21:36:53
0
francis.charles72
francis charles :
wekeni na passport kwa ushauri wangu
2026-11-19 17:26:22
0
mtumish19
penina :
nchi haina majukumu ya kufanya siku hizi
2026-11-19 19:14:45
2
user12806683508055
[email protected] :
nyienyieee haa 😳
2026-11-19 20:24:22
0
grace.karata0
Grace Karata :
Duuuuh hii kali 😂
2026-11-19 19:27:50
0
victoriamalopola6
Victoria Malopola :
makubwa
2026-11-19 19:50:35
0
missmruma
miss money 💘💞 :
Sina nida siolew na dhini nikiulizwa mbingun kwann sikuolewa nasema serikal ilisema tusio na nida atuingia kwenye ndoa🤣🤣🤣🤣
2026-11-19 19:49:33
0
hidaya.ibrahim6
Hidaya Ibrahim :
mim ambae sina mpango wa ndoa mbona hyo nida sioni kabsa mpka nakufa
2026-11-19 20:50:37
0
nicaragua_150
Nicaragua🫶🇹🇿🍓 :
😂😂 safi sana
2026-11-19 19:44:10
0
kidotyfashion
Binty kweka :
Nasisi tuliofunga bila nida naomba ndoa zetu zifutwe tuanze upya hii sio haki
2026-11-19 22:01:31
0
rukhaiydaf
Rukhaiy daff :
kwani mm ni talala na nida jamani msinipangie chakufanya
2026-11-19 22:27:37
1
s_97215087
minally :
mtajiowa wenyew
2026-11-19 20:01:17
0
roxiemanong
ms gracey :
kama nina namba tu kwahy siolewi[Tears of joy]
2026-11-19 22:05:33
0
user8347949870552
user8347949870552 :
wakiridhia wazazi' muowaji shekhe, walking na mashaid.....🙌
2026-11-19 19:40:17
0
To see more videos from user @sautiyanjombe, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About