@chawamata_tv: VIDEO: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakigomea utekelezaji wa sheria ya kukatwa pointi kwenye leseni za udereva kutokana na kutopatiwa elimu ya kutosha kuhusu sheria hiyo kabla ya kuanza kutekelezwa. Rais Samia amesema hali hiyo imejitokeza baada ya baadhi ya madereva kupinga utekelezaji wa sheria hiyo, wakieleza kutoridhishwa na adhabu zinazotolewa pamoja na utaratibu wa kupunguziwa pointi kwenye leseni zao. Akizungumza kuhusu suala hilo, Rais Samia amesema haipendezi kuona wananchi wakigomea sheria iliyopitishwa na Bunge, akibainisha kuwa changamoto iliyopo ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusu madhumuni ya sheria hiyo. Kutokana na hali hiyo, ameliagiza Jeshi la Polisi kupitia vitengo vya usalama barabarani kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi nchi nzima ili madereva waelewe kuwa sheria hiyo haijawekwa kwa lengo la kuwaadhibu pekee, bali kuhakikisha usalama wao na ustawi wa watumiaji wote wa barabara. Amesema elimu hiyo inapaswa kutolewa kwa upana zaidi ili madereva waelewe umuhimu wa kufuata sheria na kuona kuwa mfumo wa kukatwa pointi ni sehemu ya juhudi za kudhibiti ukiukaji wa sheria za barabarani. Aidha, Rais Samia amewapongeza maafisa wa usalama barabarani kwa juhudi wanazofanya kutoa elimu kupitia vipindi mbalimbali vya televisheni, huku akiwataka kuongeza kasi ya elimu hiyo na kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Katika maagizo mengine, Rais Samia ameitaka Serikali kuhakikisha kamera za ulinzi na usalama zinawekwa barabarani ili kuwabaini na kuwakamata madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani. Amesema matumizi ya teknolojia hiyo yatasaidia kudhibiti ukiukaji wa sheria na kuimarisha usimamizi wa usalama barabarani nchini. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #tanzanianews #BongoUpdates #TzUpdates #newspapers#mgeyo_updates_tz #tzupdate #habarileoupdates #bongomovie #tanzaniaweddings #breakthroughloveteam #chawamata_tv #breakingbad #breakingnewsph #TzUpdates #newspapershoot #newspapers #newspapershirt #newspaperstand #breakingnewstz #tznewspapers #jamievardy #Tanzania #tznews #habarileo

CHAWAMATA TV
CHAWAMATA TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 20 November 2026 12:21:59 GMT
59401
2937
431
159

Music

Download

Comments

aniceti.njigula
𝒶𝓃𝒾𝓈ℯ𝓉𝒾 𝓃𝒿𝒾ℊ𝓊𝓁𝒶 :
tumekaribia kugoma tena. hiyo sheria ifanyieni majaribio kwa magari ya serikali na madereva wao
2026-11-20 13:21:23
130
dullah.kader
Dullah Kader :
huyu rais wa nchi gan
2026-11-20 13:30:49
53
user3256081683452
musa ramadhan :
tuta waachia tena magari
2026-11-20 13:22:46
37
mrmsukuma1
Raja msukuma :
sheria kandamizi lazma tupinge
2026-11-20 13:07:44
41
papashinotee2
PA²SHINOTEE🇹🇿 :
yani gari bovu leceen anafungiwa dereva
2026-11-20 13:03:54
28
faharidini.yassin
faharidini yassini :
mnashindwa kutengeneza barabara zetu ziwe rafiki mnatujazia matrafiki hakuna wanachopunguza zaidi ya kuneemeka ajali zipo pale pale tengenezeni barabara maneno yanakuwa mengi
2026-11-20 13:24:15
37
shaiduathumani
cudotz :
Rais hajaambiwa kuhusu hili maana hata anachozungumza bado naona hana uelewa nacho ambacho hakitakuwi sio kila kosa unashambulia leseni ya dereva hapana mengine ni kosa la gari mfano tairi kipala ukikata point kwenye leseni na ikafungiwa tajiri atatafuta dereva mwingine aendeshe icho kipara so hapo ni kufungia hata leseni au TLB za magari yapo mambo yanayomhusu dereva mfano ulevi,speed n.k
2026-11-20 12:58:12
19
isa_swalo001
Forgiven Sinner :
hivi mungu mbn kama hatusikilizi
2026-11-20 14:47:47
4
jeff13383
jeff :
namaliza bando langu
2026-11-20 14:33:48
1
user9213483602576
kapesha :
tengenezeni barabara
2026-11-20 13:31:24
5
ashrafu9463
ASHRAFU :
huyu anamaliza lini jamani tumemchoka 😳
2026-11-20 17:15:17
0
erickmasumbuko0
erickmasumbuko749 :
nimejisikia vibaya sijui nimepitaje kwenye peji hiiii😭😭😭😭😭
2026-11-20 17:20:25
0
priscasteven
user3064406355902 :
My president[Crying][Crying][Crying]
2026-11-20 15:22:18
0
ogzangira0
OG'ZANGIRA :
Time will TELL
2026-11-20 14:50:48
1
abduliddy6007
Alhamndulillah" :
serikali inawaza madereva tu yani ..
2026-11-20 13:55:31
0
stewartlusaza
user1233783790593 :
kwanz wakatwe madereva wa serikali
2026-11-20 14:52:24
2
kakurajr
kakurajr🇹🇿 :
mmmmmh htr kilichobaki tuame nchi tu
2026-11-20 13:51:01
0
mau.gado21
mau gado :
sisi tutagoma tena
2026-11-20 14:30:55
2
rooneykiwelu167
Rooney Kiwelu :
raisi aongelei barabara zake mbovu, Au ndio kitega uchumi?
2026-11-20 14:23:33
0
mpanda488
MPANDA JR🐴 :
mama tukutoe hofu tu kua hiyo sheria hatutaki na hatutaki kukaa na watu kujadili hilo maana limepita kwahy usitumie nguvu nyingi kujieleza
2026-11-20 14:05:48
2
marsh.abdul
Marsh Abdul :
daah
2026-11-20 14:46:32
1
user1536304371194
jack der🛣 road life :
katengeneze barabara kwanza
2026-11-20 13:44:48
0
stewartlusaza
user1233783790593 :
hivi huyu ni wawap
2026-11-20 14:51:54
1
ngosha.og.truck.d
NGOSHA OG TRUCK DRIVER :
awamu hii hatutagoma tena ila tutaachana tu na hii kazi wenyewe
2026-11-20 14:31:51
1
mudymanyweletz
Mudy [email protected] :
Kukatwa point haiendani namiundombinu yetu barabara nimbovu sn
2026-11-20 14:55:41
1
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About