@wizara.ya.ardhi: DAR ES SALAAM Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kutoa huduma za Kliniki ya Ardhi katika maonesho ya TAREX 2026 yanayofanyika jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwawezesha kupata huduma mbalimbali za ardhi kwa urahisi. Kupitia kliniki hiyo, Wizara inatoa elimu kwa wananchi kuhusu usimamizi, matumizi na utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na huduma zinazohusiana na hati miliki za ardhi, ikiwemo kuwasaidia wananchi wanaohitaji kupata hati miliki. Huduma hizo ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Ardhi za kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika masuala ya ardhi, kuwasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto za ardhi sambamba na kurahisisha upatikanaji huduma za umiliki wa ardhi. Aidha, kliniki hiyo inalenga kuwasogezea wananchi huduma za ardhi karibu na kuwapatia fursa ya kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi, umiliki na matumizi ya ardhi kutoka kwa wataalamu wa Wizara. Maonesho ya TAREX 2026 yanafanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam, kuanzia Novemba 20 hadi 22, 2026. Wananchi wanakaribishwa kutembelea banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kupata elimu na huduma mbalimbali za ardhi. #tiktokviral #tiktoktanzania🇹🇿 #tiktokafrica #HudumaKwaWananchi #WizaraYaArdhi

WIZARA YA ARDHI
WIZARA YA ARDHI
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 21 November 2026 11:39:24 GMT
159
4
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @wizara.ya.ardhi, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About