@uhuruonline: #HABARI : RAIA wa Jimbo la Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wamelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa juhudi zake za kurejesha amani katika eneo hilo. Pongezi hizo zimeelekezwa kwa vikosi vya JWTZ vinavyohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO), kufuatia vitendo vya mauaji na uharibifu wa mali na miundombinu. Vitendo hivyo vinadaiwa kufanywa na vikundi haramu vyenye silaha, hali iliyosababisha wananchi kukumbwa na madhila mbalimbali, huku vikosi vya JWTZ vikiendelea kutekeleza majukumu ya kulinda amani na usalama. Katika kuimarisha ustawi wa wananchi, Kikosi cha Tano cha Utayari cha Walinda Amani wa JWTZ (TANZQRF-05) kimetoa msaada wa chakula kwa waathirika, kikisisitiza kuwa ulinzi wa amani unakwenda sambamba na huduma za kibinadamu. #uhuruonline #uhuruupdates