@vicentsimango: Harmonize amezungumza wazi kuhusu Ibraah. Ameeleza kuwa anaheshimu ombi la Ibraah la kutotaka kuzungumziwa na ndiyo maana hataki kuingia undani kuhusu yaliyotokea kati yao. Alisema kitendo cha Ibraah kumuweka ‘block’ ni jambo dogo ukilinganisha na wema aliomfanyia. Anaamini siku moja Ibraah atatambua hilo. Harmonize amesisitiza kuwa hana nia ya kumhukumu Ibraah kwani bado ni kijana na anaamini ni mtu mwema. Pia, amefafanua kuwa kufanikiwa kunahitaji bidii, maombi na neema za Mwenyezi Mungu, si pesa peke yake. Amehimiza watu wasimpe Ibraah msongo wa mawazo na waheshimu uamuzi wake wa kutotaka kuzungumziwa. Toa maoni yako. Follow KASA MEDIA. #Harmonize #Ibraah #KASA MEDIA