@tanzaniahabari: Mkurugenzi wa Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohamed Salum, amesema kuwa Muungano umejengeka katika misingi ya umoja, udugu, kuheshimiana na majadiliano. Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na kituo cha redio cha Uhuru FM.