@finishingmaster: 💡 JE, UNAJUA TAA ZAKO ZINAWEZA KUBADILISHA MUONEKANO WA RANGI KWENYE NYUMBA YAKO? Hiki ni kijumba cha kujifunza! Na kujifunza hakukomi mpaka mwaka 2026 uishe na kuingia mwaka 2027. Tunaendelea kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ujenzi na finishing za kisasa. Leo tunajifunza kuhusu ATHARI YA MUANGA WA TAA KWENYE RANGI ZA NYUMBA. Je, unajua kwamba taa ulizofunga zinaweza kubadilisha kabisa mwonekano wa rangi kwenye kuta, tiles na sehemu mbalimbali za chumba chako? Kama unavyoona kwenye video hii, ninapozima na kuwasha taa zenye rangi tofauti, mwonekano wa chumba unabadilika. Rangi za kuta na tiles zinaweza kuonekana tofauti kulingana na aina na rangi ya mwanga unaotumika. Hii ni kwa sababu mwanga wa taa unaakisiwa kwenye kuta, sakafu na vitu vilivyopo ndani ya chumba, hivyo kubadilisha taswira ya rangi tunayoiona. USHAURI WANGU: Unapopanga finishing ya nyumba yako, usichague rangi za kuta na tiles pekee. Fikiria pia aina ya taa utakazofunga, rangi ya mwanga wake na namna zitakavyoleta muonekano mzuri kwenye kila chumba. Kumbuka, taa nzuri inaweza kuongeza uzuri wa finishing yako, lakini taa isiyochaguliwa vizuri inaweza kubadilisha mwonekano uliokuwa unautarajia. Hiki ni kijumba cha Mwalimu Mr Finishing Master 101 — KIJUMBA CHA KUJIFUNZA. Tunaendelea kujifunza, kuboresha na kushirikishana maarifa ya finishing za kisasa. FINISHING MASTER – UBORA UNAONEKANA. #FinishingMaster #MwalimuMrFinishingMaster101 #ModernFinishing #LightingDesign #InteriorDesign

Finishing master
Finishing master
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 25 November 2026 16:18:04 GMT
996
29
1
2

Music

Download

Comments

arman.udg
𝐀𝐑𝐌𝐀𝐍 :
sawa
2026-11-25 16:29:53
0
To see more videos from user @finishingmaster, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About