@massoudkhaifan: Wazazi na wapendwa wetu waliotangulia mbele ya haki hawapaswi kusahaulika katika dua zetu. Ingawa hatuwaoni tena, bado tuna nafasi ya kuwakumbuka kwa kuwaombea msamaha, rehema na Pepo ya Firdaus. 🤍🕊️ Dua ni zawadi nzuri tunayoendelea kuwapa hata baada ya kuondoka kwao duniani. Tuwe watoto wema, tuwaombee daima na tuendelee kufanya mema kwa ajili yao. Allah awarehemu wote waliotutangulia, awaangazie makaburi yao na atukutanishe nao katika Pepo Yake, mahali ambapo hakuna huzuni wala kutengana tena. 🤲🏽 Aamiin Ya Rabbal-‘Aalamiin. #jumaamubarak #foryoupage #foryou #viral