@taimediatz: #HABARI Kwa miaka mingi, dhana potofu ya kwamba changamoto za uzazi huwakabili wanawake pekee imewafanya wanaume wengi kusita kutafuta msaada, huku wakisahau kuwa nao wanaweza kuwa sehemu ya changamoto hiyo. Abdallah Shaban ni miongoni mwa waliovunja mwiko huo baada ya kugundua kuwa ana changamoto ya uzazi, lakini kupitia uchunguzi na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, yeye na mke wake wamefanikiwa kupata watoto na kutimiza ndoto yao ya kuwa wazazi. ✍🏿 @mariamshabanitz #taimediatz #taimediatv