@jambotv_: VIDEO: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema kiwanda cha kuzalisha sukari cha Kasulu ndicho kitakachomaliza pengo la sukari nchini na kuifanya Tanzania ijitosheleze na kuanza kuuza sukari nje ya nchi. Akizungumza Novemba 26, 2026 wakati wa ziara yake mkoani Kigoma alipotembelea mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Mufindi Paper Mills Limited, Profesa Mkumbo ameeleza kuwa Tanzania kwa sasa inazalisha takriban tani laki nne za sukari wakati mahitaji ni tani laki sita, na kuacha upungufu wa tani 200,000 ambao kiwanda hicho kitamaliza. Profesa Mkumbo ameeleza kuwa uwekezaji wa mradi huo wa Kasulu unakadiriwa kufikia dola za Marekani milioni 320 karibu Shilingi trilioni moja, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2027, huku ukilenga kuzalisha hadi tani laki sita utakapokamilika kwa hatua zote na kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha sukari katika ukanda wa Afrika Mashariki. Profesa Mkumbo ameongeza kuwa mradi huo unahusisha mashamba makubwa ya miwa yenye teknolojia ya umwagiliaji na unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi wa Kigoma na Watanzania.
Jambo TV
Region: TZ
Friday 27 November 2026 07:53:28 GMT
Music
Download
Comments
Johnson Barobewe :
wap hap0
2026-11-28 00:34:38
0
nkezifid :
iko seem gan
2026-11-27 15:28:42
0
shebdy :
icho kiwanda wangekiita kigoma sugar
2026-11-27 17:55:18
1
bravo :
afadhali kigoma yetu sasa inaanza kupewa hadhi iliyostahili. kigoma ni lango la muhimu kukuza uchumi wa Tanzania.
msifanye kwa kila mkoa hapo ndo mnataka ku feil chunguza mikoa ya kimkakati. bila kujari ukanda.
2026-11-28 10:54:14
0
cherry :
hiz maneno hazijawahi kuisha
2026-11-28 07:04:23
0
CHEED BOY :
nawependa sana hawo laha sn
2026-11-27 12:40:28
0
lucas :
labda kwa bei hii
2026-11-27 10:51:17
1
kisiki🇹🇿 :
mhhh
2026-11-27 10:01:50
0
The white shadow :
mkiwa mnaongea , kama kweli vile😁, lakin nikikumbuka wakati bwawa la Mwal. Julius Nyerere mlisema tutazalisha umeme mwingi hadi kuzidi mahitaji yetu hadi tutauza nje ya nchi ila sasa baada ya bwawa lenyewe kukamilika bado tunanunua umeme kutokea Ethiopia kupitia kenya!😂
2026-11-28 06:33:22
1
Wilson Israel :
😳😳😳
2026-11-27 14:41:05
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.