@enochnjele: MAHUSIANO YA KIHISIA KWA SAGITTARIUS/MSHALE WALIOZALIWA:NOVEMBER 22-DECEMBER 21 1.Watu wa Sagittarius ni vigumu kuwafahamu au kuwafunga kihisia. 2.Hawapendi kuingia katika mahusiano yenye migogoro mingi au yanayowazuia kufanya mambo wanayotaka. 3.Hawapendi chochote kinachowafunga au kuwazuia kuendelea na maisha yao. 4.Una maeneo mengi ya kwenda na mambo mengi ya kufanya, hivyo hupendi kujifunga katika jambo linalokuweka sehemu moja. 5.Njia mojawapo ya kudumisha uhuru wako ni kujiepusha na hisia zinazoweza kukufunga. 6.Watu wa Sagittarius mara chache huzungumza moja kwa moja kuhusu hisia zao. Badala yake, huzungumza kuhusu wanavyofikiri juu ya hisia zao. 7.Mara nyingi, wenzi wao wa kimapenzi hushangaa wanapohitaji kuonyeshwa mapenzi, hisia na upendo wa kina zaidi. 8.Kwa sababu huwa unaacha nafasi ya kujiondoa katika mahusiano na hupendi mahusiano ya kudumu yenye kufungamana sana kihisia, wakati mwingine unaweza kujikuta ukivunja uhusiano huo. Liphongo