@jamiivoice_: SIGRADA ALISHAURI WAZIRI MKUU ASIHANGAIKE NA KERO, LEO RAIS KASISITIZA Mbunge wa Viti Maalum, Sigrada Mligo aliwahi kukumbana na upinzani mkali Bungeni baada ya kushauri kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania anapaswa kushughulikia mambo nyeti ikiwemo mikataba ya nchi kuliko kuzunguka kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Kauli hiyo ilisababisha Sigrada kukumbana na taarifa kutoka kwa Wabunge na Mawaziri wakipingana na ushauri huo. Sigrada alishauri kuwa mfumo wa utawala wa nchi una ngazi mbalimbali zinazoweza kutatua kero za wananchi kuliko kusubiri viongozi wakuu wa Serikali. Leo hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Tamisemi kushughulika na kero za wananchi na sio Waziri Mkuu kuhangaika kwenda kutatua matatizo ya wananchi. Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Novemba 27, 2026 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha Viongozi aliowateua.