@jamiivoice_: HABARI: Usiku wa kuamkia leo, Novemba 27, 2026, wafanyabiashara wa Mbezi kwa Msuguri, jijini Dar es Salaam, wamejikuta wakikabiliwa na hali ya sintofahamu baada ya vibanda vyao kubomolewa, hatua iliyozua malalamiko na hasira miongoni mwa wajasiriamali hao. Ubomoaji huo umeibua mjadala, huku Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, akijitokeza kupinga hatua hiyo na kutangaza kutoshirikiana tena na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam, kutokana na namna ubomoaji huo ulivyofanyika. Akizungumza na wananchi hao leo, Msando amesema hakuna maelekezo kutoka kwa viongozi wakuu wa Serikali yaliyotolewa kuhusu ubomoaji huo, akisisitiza kuwa hawezi kukubaliana na hatua zinazoharibu mali za wananchi wanaojitafutia riziki. "Katika hili nitatengana na yoyote ambaye anathubutu kukanyaga hati ya mwananchi. Haiwezekani wananchi wanaamka asubuhi wanakuja kujitafutia riziki hapa. Palikuwa pachafu, leo tumepaboresha, tumepasafisha, mtu anakuja kubomoa usiku," amesema Msando. Katika hatua nyingine, Msando ameliagiza Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC) kutotoa vibali vya ulinzi kwa mtu yeyote atakayetaka kufanya ubomoaji wa vibanda hivyo. Amedai kuwa TANROADS waliombwa kutoa vibali lakini hawakujibu maombi hayo, hali iliyomfanya kuitaka Kamati ya Baraza la Madiwani kukaa na kumwita mwakilishi wa wakala huyo ili aeleze sababu za kutokutoa vibali hivyo.

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 27 November 2026 18:47:29 GMT
10228
402
29
19

Music

Download

Comments

chimoo665
chimoo :
SINEMA zetu
2026-11-28 05:46:34
1
ahmedimaftaha
AHMED MAFTAHA :
mbon munatuchanganya sas km RAISI na MAKAMU WARAISI WAZIRI MKUU hajaagiza hayo mawazo yakuja kuvunja wameyapat wap au NCHI hii kwan inawatoa amri wangap
2026-11-28 07:17:20
0
angelmraha
anger :
embu toa iyo neno raisi
2026-11-28 08:47:40
1
castor.francis
Castor Francis :
lbd hamtutaki hii nchi tuhame2 tuwaachie
2026-11-28 05:06:56
0
juma.mad3
Juma :
nash ndw kuelew
2026-11-28 07:38:34
0
user9058173884034
mr raph :
mhhh Mungu atupe nguvu sana na atusaidie
2026-11-28 08:19:41
1
kasusu690
kasusu :
ni kweli unatetea wananchi au una Maslahi nao ,kwa sababu kibanda kimoja kinapandishwa zaidi ya laki sita je ni sahh
2026-11-28 06:18:17
0
tarimoone
user7437240735291 :
huyu hivi yule hivi
2026-11-28 02:43:15
0
user5214469007668
Side kapoyola :
mitano tena
2026-11-28 03:37:23
0
ndimbo25
Ndimboaminiel :
nakuonea huruma dc
2026-11-28 06:26:21
0
user7035851838335
smart boy 06 :
nashangaa sn kila mtu anajiamulia hii ni dharau kwa mwenye mamlaka mnamdharau mnagombanisha watu wamchukie
2026-11-28 04:53:08
0
riziwani58
Riziwani :
hii Tanzania hii jamani inaenda kubaya
2026-11-27 20:33:49
0
msuph.yona
Msuph :
mmmh serikali ni moja...tu.....hapo kunatatizo la leadership communication
2026-11-27 19:48:34
0
djjamespaul
dj james :
hizo ni siasa mbona sheli hazibomolewi na wamejenga ma frem kabisa ila husikii wameguswa
2026-11-27 20:12:25
0
user5211212487618
Lord Sr :
Wakuu , tuheshimu utawala wa sheria, mkuu. ungepewa ofisi hiyo usimamie bila sheria na taratibu ungeweza ?
2026-11-27 18:59:52
0
wong_quality_fabrics
J four :
SubhanAllah Allah anawaona
2026-11-27 20:53:14
0
sosovelemalipula
sosovele malipula :
duh?????,, acha ninyamaze mmm
2026-11-27 21:02:49
0
venasmoris
venas :
sema baba
2026-11-28 05:08:08
0
makamo.wa.raismgog
Makamo wa rais(mgogo) :
sijui niseme nn mm mtawala😭😭
2026-11-28 10:23:59
0
idilisaguda
Idilisa🇹🇿 :
Hawa ndo viongozi tunaowataka sisi watanzania, sio viongozi waoga waoga kwenye kuzungumza ukwelii
2026-11-28 07:08:08
0
mmmmmmmmh495
ibra💪 :
UJA ,,,, ,,,, ,,,,, MBO
2026-11-28 09:43:38
0
revocatus53
Respicius paul ndyakoa :
km hawajahagizwa limefanyikaje hacha kungata na kuriza wauni tuu
2026-11-28 08:48:27
0
makambajohnmakamb
Makamba john Makamba john :
hawao ndio wanampa lawama mama
2026-11-28 06:55:59
0
.steven76
STEVEN🦋 :
Tanroad wahuni
2026-11-28 05:10:02
0
fahadsimkoko
Memes :
sasa tutajuaje vikao vyao vya ndani kama hawajaaagizaga
2026-11-28 05:08:45
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About