@mozannah: Assalam alaykum guyyysss... Haya leo njooni tupike vibibi pamoja na rojo lake😍😍💃 Tunaanza na vibibi , Mahitaji yake ni -Mchele wa VIP nusu kg -Hamira unaweza ukaweka 1tbspn mi nimeweka hiyo pakt 1. -Hiliki -Wali uliopikwa 3 tbspn -Sukari 3 tbspn -Tui la nazi mls 750 (Hicho kikombe ni 500mls) nimeweka kimoja na nusu Utasaga mpaka ulainike vizuri utaacha uumuke. Utavipika na ukimaliza ndio utapika rojo lake sasa😍😍 Rojo la vibibi😍 -nusu lita tui la nazi, Nimeweka nusu nazi tui bubu na nazi 2 za pakt pamoja na maji mpaka kikombe kijaaa vizuri. -Maziwa ya unga 2 tbspn -Sukari utakisia unavopenda -Chumvi kidogooo -1 tbspn corn flour utamix na maji nusu kikombe -Hiliki Utapika na ukiona imekuwa uzito sawa utaitoa jikoni tayari kwa matumizi😍 Bye guyyysss... Enjooyyy🩷🩷🩷 #viral #trend #creatorsearchinsights #swahili