@miss_lovely74: Kujitambua si kushindwa kujibu kila unapoumizwa, wala si kushindwa kutetea ukweli wako. ..Ni kufikia hatua ambayo unatambua kuwa si kila jambo linahitaji majibu yako, si kila mtu anastahili maelezo yako, na si kila mabishano yana thamani ya muda wako.. Wakati mwingine unaweza kujua ukweli wote, ukawa na ushahidi wa kujitetea, lakini ukaamua kunyamaza kwa sababu unathamini amani yako kuliko kushinda mabishano.. Ujumbe :🦋Usiruhusu tabia za watu zikunyang'anye utulivu wa moyo wako... Kujua wakati wa kuzungumza na wakati wa kunyamaza ni hekima..