@jose_chikunde: Hakuna mtoto aliyezaliwa na tabia mbaya au nzuri, wote wamepata tabia zao kutokana na malezi na mazingira waliyokulia na kulelewa. Watoto wa Kiafrika wanatakiwa wafuatiliwe hadi wafike 21 au hata zaidi ndipo waachiwe kujiamulia mambo yao wenyewe. Wazazi na walezi sikuhizi tumekuwa bize ktk kutafuta pesa na kuwaachia wadada wa kazi malezi ya watoto. Tunafikiri kuwajazia soseji ndio kuwapenda kumbe tunajaribu afya zao na future yao. Aliyewaambia wanawake kuwa kutoka nyumbani alfajiri na kwenda ktk kazi ya kuajiriwa ni ‘kuwa huru na wa kisasa’ lakini kukaa nyumbani na kulea watoto wao ni kuwa mfungwa, aliwaweza sana.