@winstone_nnko: Kama wewe ni fundi na unataka kufanya installation ya solar kwa matumizi ya DC, hii set-up inafanya kazi vizuri. Inakuwa na hizi components: - Solar panels. Zinabadilisha mwanga wa jua kuwa umeme wa DC - DC circuit breaker. Inakata umeme wakati wa fault au overload ili kulinda mfumo - DC surge protective device. Inalinda mfumo dhidi ya mshtuko wa umeme wa ghafla kama radi. - Earth rod. Inapeleka hitilafu ya umeme ardhini kwa usalama - MPPT charge controller. Inasimamia kuchaji battery kwa ufanisi na kuongeza output kutoka panels. - Battery. Inahifadhi umeme kwa matumizi ya baadaye. - Inverter. Inabadilisha umeme wa DC kuwa AC kwa ajili ya vifaa vya kawaida. Kila kifaa kina mchango wake kwenye usalama, ufanisi, na utendaji wa mfumo mzima. Kwa sasa kuna hybrid inverter yenye charge controller ndani yake, lakini gharama yake ipo juu kidogo lakini unaweza kuitumia kama mteja yuko vizuri financially.