@lochamedia: Shabiki mmoja mkubwa wa Cristiano Ronaldo amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonyesha jinsi alivyosherehekea bao la nyota huyo dhidi ya Croatia bila kumuamsha mke wake aliyekuwa amelala. Katika video iliyosambaa mtandaoni, shabiki huyo alidhibiti hisia zake kwa kushangilia kimya kimya badala ya kupiga kelele, jambo lililowavutia wengi kwa ubunifu wake na kuonyesha namna alivyoweka kipaumbele utulivu wa familia yake huku akiendelea kufurahia mchezo.