@daarularqamonlinetv: RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI KATIKA MAZIKO YA SHEIKH SAID OTHMAN AL KADIRY ‎Daarul Arqam Tv ‎ ‎Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali katika maziko ya Sheikh Said Othman Al Kadiry, aliyefariki dunia tarehe 7 Julai 2026. ‎ ‎Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alishiriki Sala ya Jeneza iliyosaliwa katika Msikiti wa Ijumaa wa Tunduni kwa Masharifu, Mkoa wa Kaskazini Unguja. ‎ ‎Marehemu Sheikh Said Al Kadiry, amefariki akiwa na umri wa miaka 88, alikuwa mwanazuoni mashuhuri wa dini ya Kiislamu, mlezi na msimamizi wa Tariqatul Qadiriyya nchini. ‎ ‎Marehemu amezikwa kijijini kwao Tunduni Mchangani. ‎ ‎Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi. Amina. ‎#daarularqamonlinetv ‎#fyp #zanzibar #tanzaniantiktok🇹🇿 ‎#follow

@daarul_arqam_online_tv
@daarul_arqam_online_tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 09 July 2026 18:42:08 GMT
924
59
1
1

Music

Download

Comments

abudaudi333
abudaudi2020 :
allah amrahamu kipenz chetu
2026-07-09 20:28:44
0
To see more videos from user @daarularqamonlinetv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About