@veriafya: Akizungumza kupitia TBC Online, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi anaeleza kuwa udumavu huanzia tumboni mwa mama mjamzito asiyepata lishe bora, na baada ya kuzaliwa, tatizo hili huongezeka kutokana na kuacha kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo na badala yake kutumia maziwa ya kopo au kuwapa vyakula mapema, jambo linalosababisha magonjwa ya kuhara kutokana na ukosefu wa usafi. Anafafanua kuwa ingawa kiwango cha udumavu nchini kimeshuka hadi asilimia 31, bado kipo juu ya kiwango kinachokubalika kimataifa (chini ya 30%), na athari zake kwa ukuaji wa akili na mwili ni vigumu kurekebishwa.