@johnymnaku: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema dunia inaingia katika “eneo hatarishi” la hali ya hewa kutokana na kuimarika kwa El Niño, inayotarajiwa kufikia kiwango cha juu mwishoni mwa mwaka huu. Guterres amesema ongezeko la joto la bahari na kupanda kwa joto duniani vinaashiria hatari ya kuongezeka kwa matukio ya hali mbaya ya hewa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema El Niño imeimarika na inatarajiwa kuwa na nguvu kubwa katika miezi ijayo, huku hali hiyo ikitarajiwa kuendelea hadi Februari. Shirika hilo limeonya kuwa athari zake katika mifumo ya joto na mvua zinaweza kuendelea hadi mwaka 2027. Kwa mujibu wa WMO, kuimarika kwa El Niño kunaweza kuongeza hatari ya mafuriko, ukame na joto kali katika maeneo mbalimbali duniani. Ingawa El Niño ni hali ya asili ya tabianchi na haisababishwi na mabadiliko ya tabianchi, wataalamu wanasema inaweza kuchochea zaidi joto na matukio ya hali mbaya ya hewa katika sayari ambayo tayari inapata joto kutokana na uchomaji wa nishati za mafuta. Guterres amesema dunia iko katika mazingira ambayo hayajawahi kushuhudiwa, akitaka mataifa kuongeza kasi ya kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda jamii dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza. Amesema ushindani uliopo sasa ni kati ya kuongezeka kwa hatari za hali ya hewa na kasi ya hatua zinazochukuliwa kuwalinda watu. #AzamTVUpdates Mhariri | John Mbalamwezi

johny
johny
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 03 September 2026 13:16:56 GMT
3218
53
0
3

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @johnymnaku, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About